Sasa ni wazi kuwa wawakilishi wa
Tanzania katika michuano ya vilabu ya kombe la Shirikisho barani Afrika,
Yanga watacheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika raundi ya pili ya
michuano hiyo.
Yanga imefanikiwa kuwatoa Platinum FC licha ya
kufungwa 1-0 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Bulawayo, nchini
Zimbabwe. Hii inafuatia ushindi wa 5-1 ambao Yanga uliipata katika mechi
ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Tanzania.Vigogo hao wa Tunisia, wenye uzoefu wa kucheza michuano mikubwa Afrika, imepata nafasi ya kucheza na Yanga baada ya kutoka sare ya 1-1 na timu ya Benfica de Luanda. Katika mechi ya kwanza, Watunisia walishinda 1-0.
Kocha wa Yanga, Mdachi Hans Pluijm atakuwa na kibarua cha ziada kuwahkikisha wanasonga mbele huku nahodha wake, Nadir Haroub “Cannavaro” akisema wapo tayari kucheza na timu yoyote katika michuano hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni