23 Aprili 2015

Bastola ya Ray Yazua Hofu Ukumbini

Bastola ya Ray Yazua Hofu Ukumbini
Staa wa Bongo Movies Vincent Kigosi ‘Ray’  adaiwa kuzua hofu ya aina yake baada ya kutinga fulana fupi iliyosababisha silaha yake aina ya bastola kuonekana na
kuwafanya watu waliomzunguka kujawa na hofu.
Gazeti la Risasi limeripoki kuwa tukio hilo la aina yake lilitokea Jumamosi iliyopita katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na uzinduzi wa video ya wimbo wa Nashindwa wa mwanamuziki Christian Bella.
Mwanahabari wa gazeti hilo aliyekuwa akikusanya matukio ukumbini humo, aliwashuhudia watu waliomzunguka Ray wakionesha hofu yao  pale fulana yake ilipopanda juu na kuiacha bastola yake aliyoichomeka kwenye suruali ikionekana bila kificho ambapo zaidi walihofia mazingira ya unywaji wa pombe uliokuwepo.
“Jamani hii si hatari na ‘masanga’ haya anayogonga hapa ukimkorofisha hata kidogo tu si anaweza kukushuti bila kuwaza nini kitatokea?,” alisikika mmoja wa watu waliokuwa wamekaa jirani na msanii huyo.Baadhi ya watu hao waliokuwa jirani na Ray aliyekuwa amekaa pamoja na msanii mweziye Jacob Steven ‘JB’, walionekana wakiondoka eneo hilo kwa hofu ya usalama wao.
Hapa si salama sana ndugu zangu bora tuondoke, unaweza hata ukamkanyaga bahati mbaya akakulipua makusudi,” alisikika jamaa mwingine aliyekuwa eneo hilo.Jitihada za mwanahabari wetu kuzungumza na Ray eneo hilo hazikuweza kuzaa matunda kufuatia mazingira ya unywaji pombe uliokuwepo, lakini alipotafutwa siku iliyofuata, simu yake iliita bila kupokelewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728