09 Aprili 2015

MAMBO YA SIASA

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ameshiriki kikamilifu kubomoa misingi ya taifa hili. Ni kutokana na kutaka kuwapo Mahakama ya Kadhi nchini. Anaandika Eberi M. Manya … (endelea).
Ameahidi ndani ya Bunge Maalum la Katiba, kuundwa kwa mahakama hii na sasa anajitahidi kadri awezavyo kuhakikisha inapatikana sasa.
Siyo kesho wala kesho kutwa. Muswada juu ya mahakama hiyo, uko njiani kuingia bungeni.
Pinda anasema, Mahakama ya Kadhi itakayoundwa, itashughulikia mirathi na ndoa. Basi!
Wapo wanaofananisha harakati za Pinda za kutaka kuingiza Mahakama ya Kadhi nchini na mbio zake za kusaka urais kama alivyoeleza katika tangazo lake la kimyakimya.
Ikiwa ni hivyo, basi atakuwa anafanya makosa makubwa sana. Urais haupatikani kwa kughiribu Waislamu. Urais unapatikana kwa mtu kuwa mkweli, mwadilifu na mwenye uwezo wa kusimamia kile unachokinena. Pinda hana sifa hizo.
Pinda tayari amelikoroga. Kauli yake kuwa Zanzibar sio nchi, ni kikwazo kingine katika mbio zake hizi. Kuruhusu kuwapo Mahakama ya Kadhi ndani ya mgawanyiko kati ya waumini wa Kiislamu na Kikirsto, ni kutenda makosa kama ambayo, Rais Yoweri Museveni aliyafanya nchini kwake mwaka 1986. Alirejesha utawala wa kifalme katika eneo la Baganda. Utawala wa Kabaka ulikuwa umefutwa na watangulizi wake. Museveni alidhani kumpa Kabaka hadhi yake ya ufalme, kungesaidia kuishi kwa amani zaidi.
Miaka minne baadaye, maafisa wa mamlaka ya kodi walipoenda Buganda kukusanya kodi katika eneo hilo ambalo linahusisha jiji la Kampala, wakaambiwa Rais Museveni hana mamlaka juu ya eneo hilo. Kodi wakasema wanalipa kwa Kabaka.
Tatizo hilo bado lingalipo hadi leo. Serikali inalazimika kupigana vita ya ndani kwa ndani kwa sababu tu mfalme Kabaka hatambui mamlaka ya serikali.
Tunafahamu “sakata” la mahakama ya Kadhi lilipoanzia. Limeletwa na serikali ili kuwalainisha Waislamu, kupigia kura ya “Ndiyo” Katiba pendekezwa.
Yawezekana dhamira ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ilikuwa njema, lakini mkondo iliyopitia kutaka kuiunda, haukubariki.
Mahakama hii inaletwa kama rushwa kwa Waislamu.
Hatua ya hukumu za mahakama hiyo kusajiliwa katika mahakama kuu au waziri mwenye dhamana na masuala ya sheria kuthibitisha maamuzi ya mahakama hiyo, ni kuingiza dini katika utendaji wa serikali.
Dini zote zinapaswa kujiendesha kwa sadaka au michango ya waumini wao. Kama Mahakama ya Kadhi itaanzishwa, kuna siku serikali italazimika kuidhinisha, kulipia na kugharamia mahakama za makanisa.
Aidha, kuruhusu ujio wa Mahakama ya Kadhi, tena kufanya kazi zake kwa kutumia kodi za wananchi wote, kutachagiza, kufunguliwa milango kwa Wakristo kutaka kesi zao ziishie madhabahuni.
Ndani ya Kanisa Katoliki kwa mfano, kuna sheria – Canon  Laws – ambazo ni kali mno. Wakristo wanaokengeuka huadhibiwa kwa kunyimwa huduma zote za kanisa  (excommunication).
Tukifikia hapo nchi hii haitatawalika tena.  Maelezo kwamba kesi za Waislamu zikihukumiwa na mahakimu au majaji wakristo hawazifahamu vyema sheria za Kiislamu hayana mashiko. Sheria za Kiislamu au (Islamic Law) kwa yeyote aliyesoma sheria anaisoma.
Mfumo wetu wa kutoa haki ambao Ibara ya 107 A ya Katiba ya Jamhuri tumeitumia kwa miaka zaidi ya 50 sasa, hakujawa na kasoro, zinazohalalisha kuundwa kwa mahakama hii.
Tukiingiza imani katika uendeshaji wa nchi kwa matarajio kuwa ama tutapigiwa kura na Wakristo au Waislamu; ama mtu kutaka urais, tutaitumbukiza nchi katika vurugu.
Ni bora Pinda akose urais ikiwa nia yake ni hiyo; lakini taifa libaki salama.
Tayari maaskofu wameshatoa tamko lao la kupinga mahakama ya kadhi. Nimesikia baadhi ya viongozi wanawabeza.
Mwandishi wa makala hii, amejitambulisha kuwa ni msomaji wa mtandao huu na mtafiti wa masuala ya kisiasa. Anapatikana kwa simu namba 0785 510536, barua pepe: ebermanya@yahoo.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728