Dar es Salaam. Upungufu wa chakula kwa baadhi ya mikoa nchini
umeendelea kusababisha ongezeko la mfumuko wa bei wa Taifa kutoka
asilimia 4.2 hadi asilimia 4.2 ndani ya mwezi mmoja.
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraimu Kwesigabo, aliwaambia waandishi wa
habari leo kuwa, kutokana na upungufu huo bei za bidhaa za vyakula
zimeongezeka.
“Mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka
unapimwa kwa kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma
zote zinazotumiwa na kaya binafsi,”alisema.
Aliongeza: “Hivyo kutokana na ongezeko la bei za
bidhaa hizo pamoja na huduma zote kwa kaya zimesababisha mfumuko wa bei
wa taifa,”alisema Kwesigabo.
Aliendelea kueleza kuwa, kasi ya upandaji wa bei
za bidhaa hizo zimesababisha mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi iliyopita
kuongezeka hadi ukufikia asilimia 4.3 kutoka asilimia 4.2 ya mwezi
Februari mwaka huu.
Kwesigabo alisema, ongezeko la mfumuko wa bei kwa
mwezi Machi umesababishwa hasa na kuongezeka bei za bidhaa za vyakula
kwa kipindi kilichoishia Machi mwaka huu tofauti na ilivyokuwa kwa Machi
mwaka jana.
Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mchele, unga wa muhogo, nyama, samaki, maharage, choroko na sukari.
Alisema kutokana na hali hiyo wananchi wataendelea
kushuhudia bei za vyakula zikiendelea kupanda na kwamba bei waliyokuwa
wakinunua bidhaa za vyakula hapo awali itabadilika.
Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa
mwezi uliopita ikilinganishwa na mwezi Septemba, 2010 alisema, uwezo wa
Sh 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh 64 na senti 15 mwezi
Machi mwaka huu kutoka Septemba, 2010.
“…ikilinganishwa na Sh 64 na senti 59 ilivyokuwa Febriari mwaka huu,”alisema Kwesigabo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni