23 Aprili 2015

Je, umewahi kula mishikaki ya chura?

Kwa wapenzi wa kula nyama choma na hususan mishikaki katika vituo vya mabasi, mnatakiwa kuwa makini na nyama choma hiyo kwani waweza kula mishikaki ya paka, mbwa, nyoka na
sasa mishikaki ya nyama ya chura.
Mishikaki ya nyama ya chura
Philip Paul ni muuzaji wa nyama choma za chura - na yeye pamoja na mke wake na mtoto wao wa kike wanapenda kula mishikaki ya chura. Familia hiyo inatoka jimbo la katikati ya Nigeria la Benue lakini wanaishi kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambako watu hawapendelei nyama hii ya chura.
Philip mwenye umri wa miaka 25 anasema ni rahisi kuwakamata vyura kwa mikono mitupu. Usiku anawatega kwa kuwawekea popo na vyura wanaporuka huwaendea na kuwakamata.
Baadaye anawatunga katika mti. Tangu mwaka 2008 amekuwa akifanya biashara kwa kuwakamata vyura katika jimbo la Adamawa na kuwasafirisha kwenda jimbo la Benue, ambako mishikaki ya chura inapendwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728