Mchezaji wa zamani wa ligi kuu ya premia ya Uingereza Andrea Dossena amekamatwa kwa kuiba bidhaa dukani.
Mchezaji
huyo wa zamani wa klabu ya Leyton Orient anadaiwa kuwa aliiba katika
duka moja la kifahari la Harrods lililoko jijini London.Awali Andrea aliwahi ichezea timu ya Liverpool.
Andrea alikamatwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha Brompton Road, Knightsbridge.
Andrea alikamatwa akiwa na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 31.
Hata hivyo waliachiliwa kwa dhamana hadi mwishoni mwa mwezi huu.
Dossena alijijengea sifa si haba alipokuwa Anfield , ikiwa ni pamoja na kuifungia dhidi ya Manchester United na Real Madrid .
Liverpool ilitoa pauni milioni saba mwezi Julai 2008, kumsajili Dossena .
Raia huyo wa Italia ameiwakilisha nchi yake katika mechi 10 alijiunga na Napoli januari mwaka wa 2010
Aidha aliwahi ichezea Sunderland mwaka 2013-14.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni