09 Aprili 2015

Mgomo wa madereva nchi nzima wanukia

Madereva wa vyombo mbalimbali vya moto, wanakusudia kushiriki mgomo wa nchi nzima Ijumaa wiki hii, kuishinikiza serikali kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika pamoja na agizo la kutaka kwenda kusoma.
Wakizungumza kupitia Katibu wa Muungano wa vyama vya madereva Bw. Rashid Saleh, Madereva hao wameiambia East Africa Radio kuwa suala la kurudia kusoma kila wanapohuisha leseni zao ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama kibao kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali.

Katibu huyo wa Muungano wa Vyama vya Madereva ameitaja kero nyingine kuwa ni hatua ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kutamka hadharani kuwa vyeti walivyonavyo madereva hao sio halali na kwamba Ijumaa wiki hii wanakusudia kukutana na Waziri wa Kazi na Ajira kwa ajili ya kuzungumzia kero hizo kwa lengo la kuepusha kutokea kwa mgomo huo.
Saleh ametaja madereva wanaounda muungano huo kuwa ni wa bodaboda, bajaj, teksi, daladala, mabasi ya safari fupi, mabasi ya safari ndefu na za nje ya nchi pamoja na madereva wa magari yote ya mizigo.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa muungano wa madereva, mkutano wa Ijumaa ndio utakaoamua iwapo madereva hao wagome au waendelee na kazi kwani wamechoka kudharauliwa hata kwa mambo ya msingi yanayogusa maisha yao.
Baadhi ya dharau alizozitaja ni pamoja na wamiliki wa mabasi (yaani waajiri wao) kuwaita wao ni wahuni ilhali ni watu wazima, wenye familia, wanaofanya kazi halali na wanaohitaji kuheshimiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728