09 Aprili 2015

Ajali: Mabasi ya Ngorika na RATCO yamegongana uso kwa uso na kusababisha vifo

Name:  IMG-20150409-WA0008.jpg
Views: 0
Size:  119.7 KB
Watu 10 wamekufa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata katika Kijiji cha Mbweni Wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya jana.
Name:  Screenshot from 2015-04-09 13:47:40.png
Views: 0
Size:  437.3 KB

Polisi mkoani Tanga wamethibitisha tukio hilo na kusema ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es Salaam kwenda Tanga na Arusha.Name:  IMG-20150409-WA0003.jpg
Views: 0
Size:  149.7 KB

Kwa mujibu wa Jeshi hilo gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la RATCO lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam.

Baada ya Basi la RATCO kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Kampuni ya Ngolika lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda jijini Arusha.

Kati ya watu 10 waliokufa wanaume ni watano akiwemo Dereva wa gari dogo na Dereva wa basi la Kampuni ya Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728