28 Aprili 2015

Ashtakiwa kwa kumtia mimba mwanawe

Mahakama moja mjini Bungoma nchini Kenya imemshtaki afisa mmoja wa wadi ya Bukembe kwa kulala na mwanawe wa kike mwenye umri wa
miaka 14 kwa zaidi ya miaka miwili baada ya mkewe kufariki mwaka 2013.
Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya,mwathiriwa ambaye ni mjamzito wa miezi minne amesema kuwa mshukiwa huyo ambaye ni babaake amekuwa akimlazimisha kufanya mapenzi naye kila usiku na kumuonya kwamba angemdhuru iwapo angemwambia mtu yeyote.
''Babaangu pia ameninyima fursa ya kwenda katika shule ya upili licha ya mimi kufanya vyema katika mtihani wa KCPE. Mwaka 2013,nilifanya vyema lakini akanilazimisha kurudia darasa. Mwaka jana nilifanya vizuri zaidi lakini anadhani kwamba iwapo nitajiunga na shule ya upili ya bweni,nitamkosesha fursa ya kufanya tendo la ngono nami'',.Mwathiriwa aliiambia mahakama.
Hakimu mwandamizi Peter Ireri alimwachilia mtuhumiwa kwa dhamana ya shilingi laki moja ama pesa taslimu shilingi elfu ishirini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728