Jaji
mmoja na wakili ni miongoni mwa watu waliouawa baada ya mshukiwa mmoja
kuwafyatulia risasi ndani ya mahakama moja mjini Milan nchini Italia.
Maafisa wa idara ya mahakama wanasema kuwa mshukiwa aliyefyatua risasi ni mtu mmoja aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kutangazwa kufilisika.
Mtu wa nne anaaminika kufariki kutokana na mshtuko wa moyo.
Haijulikani jinsi mshukiwa huyo alivyoweza kuingia ndani ya mahakama hiyo huku akiwa na bunduki, kwa kuwa wageni wote hupitia vifaa vya kuwakagua ikiwa wana silaha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni