20 Aprili 2015

Aunt Amwaga Machozi Kulaaniwa Kifo

Aunt Amwaga Machozi Kulaaniwa KifoStaa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel amejikuta akidondosha machozi ya uchungu baada ya shabiki mmoja kujitokeza kwenye mtandao wa kijamii na kumlaani kifo.
Tukio hilo lilitokea juzikati baada ya Aunt kuweka picha iliyomuonyesha akiwa na Wema kwenye mtandao wa Instagram akiwa ameshika tumbo lake ndipo mfuasi wa mtandao huo anayetumia jina la Said Ulimwengu alipoibuka na ‘kukomenti’ kuwa mtoto atakayezaliwa atakuwa amelaaniwa na hata akijifungua afe na kiumbe chake.
Ujumbe huo ulisomeka hivi: “Yani ukijifungua naomba ufe na mimba yako maana utakachokizaa kimeshalaaniwa.”
Chanzo makini cha GPL kimeeleza kuwa, kitendo cha shabiki huyo kuandika maneno hayo mtandaoni kilimkwaza sana Aunt na kujikuta akibubujikwa na machozi sambamba na kushukwa na presha lakini bahati nzuri alikunywa dawa za kuipandisha, akarejea katika hali yake ya kawaida.
“Ilikuwa hatari kweli, presha ilishuka sana lakini bahati nzuri alikuwa na dawa za kupandisha akanywa ndiyo akakaa sawa,” kilisema chanzo hicho.
Aunt alipotafutwa kuhusiana na habari hiyo alikiri kutokea na kudai amejisikia vibaya sana shabiki huyo pamoja na mashabiki wengine kupenda kujadili tumbo lake.
“Najua ni wengi wanatamani kuniona sipo lakini kila kitu ni Mungu atapanga na si binadamu yeyote hapa chini ya jua,” alisema Aunt.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728