28 Aprili 2015

Raia wa Uganda kupewa mafunzo ya kijeshi


Rais Yoweri Museveni wa Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameviagiza vikosi vya usalama kuanza kutoa mafunzo ya kijeshi kwa raia kama njia mojawapo ya kupigana vita dhidi ya
kundi la kigaidi la Al Shabaab.
Amesema kuwa baada ya kundi hilo kushindwa na vikosi vya usalama vya umoja wa mataifa nchini Somalia,limeanza kuwashambulia raia wa kawaida na maeneo yasio na ulinzi,kama vile shambulizi la West gate na lile la Garissa nchini Kenya.
Kundi la Alshabaab pia lilitekeleza mashambulizi ya mabomu katika eneo la Kampala mwaka 2010 na kuwaua watu 70 waliokuwa wakiangalia mechi ya kombe la dunia.
Rais Museveni amewataka polisi ,jeshi na maafisa wa ujasusi kuwafunza raia wa Uganda ili kuwawezesha kuwalinda.

Wapiganaji wa kundi la Alshaabab

Kulingana na msemaji wa jeshi la Uganda Luteni Paddy Nkunda lengo lao sio Al Shabaab pekee.
Amesema kuwa sera hiyo inalenga kuwatuliza raia wenye ufahamu wa maswala ya usalama lakini hakuna atakayepewa silaha.
Maafisa wa serikali bado wanafanya mipango kuhusu ni lini mafunzo hayo yataanza pamoja na maelezo yao.
Kumekuwa na tamaduni ya wanafunzi wa shule za upili kupewa mazoezi wanapomaliza shule lakini mpango huo ulisitishwa katika miaka ya hivi karibuni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728