Ester aliingia hotelini hapo akiwa amevaa shati tu na kuacha wazi eneo la kuanzia mapajani, kitendo kilichowafanya wanaume wengi kuacha shughuli zao na kumkodolea macho.
“Hee! Huyu ni Ester yule msanii wa filamu? Mama yangu weee, ndo’ kavaa kivazi gani kile sasa. Yaani huyu ipo siku atatembea uchi,” alisikika akisema kijana mmoja aliyeonekana ni mfanyakazi wa hoteli hiyo.
Hata hivyo, licha ya wanaume kumpa wakati mgumu huku wengine wakimpigia miluzi na kumuita, yeye aliendelea na hamsini zake ambapo alikwenda upande wa ufukweni na kujiachia zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni