Staa mrembo kutoka Bongo Movies Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameamua kutoboa kile alichokiita kama faraja yake kwa hivi sasa.
“Faraja YANGU...Nishalia sana,nishaumia sana lakini kwa sasa
nikiona mmoja kati ya hawa analia au kuumia ndo kitu kinachoweza
kuniumiza zaidi...!MUNGU awatunzeeee”-Lulu aliandika hayo jana usiku kwenye ukursa wake mtandaoni mara baada ya kuweka picha ya mama yake na mdogo wake.
Kufuatia andiko hilo komenti za mashabiki wengi zilielekea zaidi
kumzungumzia kifo cha Steven Kanumba kwani leo tarehe 7 mwezi huu ni
siku ya kumbukumbu cha kifo cha staa huyo wa Bongo Movies ambae alikuwa
na mahusiano ya kimapenzi na Lulu.
Japo kuna baadhi ya watu amabo sio wastaarabu wamekua
wakimshabuliaLulu kwa maneno makali, lakini kwa maneneo hayo ya Lulu
nadhani wenye busara wamekuelewa.
07 Aprili 2015
Lulu: Nilishalia Sana, Nishaumia Sana Lakini Kwasasa
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni