Mwanamume mmoja kutoka upande wa
kaskazini magharibi mwa Pakistan ,amempiga risasi mpenzi wake wa zamani
na watu tisa wa familia ya mwanamke huyo mwishoni mwa wiki ;hata hivyo
inaelezwa kuwa mwanamume huyo miezi sita iliyopita aliwaua wazazi wake
pamoja na kaka zake wawili kwa kosa la kukataa kumlipia mahari.
Kijana
huyo mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 25,ambaye polisi wamemtaja kwa jina
la Mir Ahmad Shah,ambaye alikuwa mafichoni baada ya kufanya shambulizi
la kutumia silaha kwa kutumia bunduki aina ya AK-47 katika wilaya ya
Charsadda jimbo la Khyber Pakhtunkhwa.Inaelezwa na mkuu wa polisi wa wilaya hiyo chief Shafiullah Khan, kuwa Ahmad aliivamia nyumba hiyo na kuwapiga risasi watu wa familia moja waliokuwa usingizini ,na kuongeza kusema kwamba watoto wawili na wanawake wane ni miongoni mwa waliouawa.
Khan amesema kwamba Shah alikuwa akisakwa kwa kesi ya mauaji ya nduguze ,mauaji aliyoyatekeleza mwaka wa jana ,familia ya Ahmad ilikataa kukubali mahari waliyotajiwa na wakwe zao ,baba wa mchumba wa kijana huyo ambaye sasa ni marehemu walitaka kiwanja cha makazi kama mahari ya binti huyo.
Polisi mwingine mwenye dhamana Gulzar Khan,amesema kwamba baada ya kijana huyo kuitekeketeza familia yake kwa mtutu wa bunduki, aliwageukia wakweze na kuwakosea adabu kwa mahari waliyoitaka kwao.
Polisi mpaka sasa wameamua kuimarisha ulinzi mipakani na katika maeneo ambayo kijana huyo angejaribu kutafuta hifadhi, na wameapa kumtia mkononi.
Ndoa nchini Pakistan hupangwa ,na mara nyingi maharusi huwa ni mabinamu.wazazi wa mwanamke wakati mwingine hudai mahari kubwa kama bima endapo ndoa yaweza kuvunjika kwa talaka.
Kulingana na jamii zingine,mahari katika dini ya kiislam hulipwa na mwanamume ama familia ya kijana kwa kumpa bi harusi wakati wa harakati za ndoa,na mahari hiyo yaweza kuwa zawadi ama pesa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni