22 Septemba 2016

Je unavitambua vyuo vikuu bora duniani?


Chuo kikuu cha Oxford UingerezaChuo kikuu cha Oxford kimeibuka kidedea katika orodha ya vyuo vikuu bora duniani ya Times Higher Education. Hi ni mara ya kwanza kwa chuo kikuu cha Uingereza.
Oxford imeisukuma katika nafasi ya pili, California Institute of Technology, ambayo imekuwa ikiongoza orodha hiyo kwa miaka mitano iliopita .

Katika orodha ya vyuo vikuu bora barani Afrika, chuo kikuu cha Cape Town kimeibuka wa kwanza kutoka Afrika kusini kwenye orodha hiyo ya Times Higher Education.
Inadhihirisha umahiri wa taifa hilo, ambalo vyuo vyake vikuu 6 vipo katika nafasi za vyuo vikuu 15 bora kikwemo chuo cha Witwatersrand katika nafasi ya pili, Stellenbosch nafasi ya tatu, tChuo kikuu cha KwaZulu-Natal katika nafasi 5 na chuo kikuu cha Pretoria katika nafasi ya sita.
Chuo kikuu cha MakerereMakerere kilichopo Uganda ndiyo chuo kikuu nje ya Afrika kusini kufanikiwa kuwa atika nafasi ya nne.
Vyengine ni chuo kikuu cha Ghana katika nafasi ya 7, na chuo kikuu cha Nairobi katika nafasi ya 8.
Orodha ya Times Higher Education duniani inapima vitu kama mafunzo, utafiti, na mtazamao wa kimaaifa - kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaotoka nje na wafanyakazi.
Nico Cloete, mkurugenzi wa taasisi ya Higher Education Trust na mratibu wa utafiti wa elimu ya juu na Advocacy Network in Africa, anasema taasisi hizo nne katika orodha ya Afrika - Cape Town, Makerere, Nairobi na Ghana - "zimeidhinisha mipango ya kuwa vyuo vikuu vinavyoongoza kwa utafiti" nchini mwao na vimeshuhudia "ongezeko kubwa kwa wanaofuzu kwa ushahada ya uzamifu na kuunda taasisi za utafiti katika miaka mitano iliopita".

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728