22 Septemba 2016

Rais wa Botswana ''amtaka Mugabe kujiuzulu''

Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert MugabeRais wa Botswana Ian Khama amemtaka mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu mara moja kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Ameambia Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana na changaomoto za kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.
''Ni wazi kwamba umri wake na hali ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza kulinusuru taifa hilo''.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.

Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.
Khama anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728