22 Septemba 2016

Jeshi la Syria limetangaza kuanza tena mapigano makali

Mapigano mapya SyriaJeshi la Syria limetangaza kuwepo kwa mapigano mapya makali, kutaka kurudisha eneo linalodhibitiwa na waasi huko Aleppo, ambako takriban watu laki mbili na nusu wamezingirwa.
Jeshi hilo limewataka pia raia kujiepusha kuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.
Limesema njia za kutoka katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi zimewekwa wazi kuruhusu watu kutoka.
Tangazo hilo limekuja siku chache baada ya
kushambuliwa kwa eneo hilo linalodhibitiwa na waasi, mashariki mwa Allepo.
Katika hatua nyingine Marekani na Urusi zimeshindwa kukubaliana jinsi ya kuufufua upya mkataba wa kusitisha mapigano, nchini Syria.
Akizungumza baada ya mkutano wao mjini New York, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry amesema Urusi inatakiwa kuonesha umakini wake katika kumaliza ghasia nchini Syria.
''.. Iwapo Urusi itatujia na mapendekezo yenye kujenga tutawasikiliza. Watu wanahitaji kuamini kwa vyovyote vile inastahili kubadilisha mbinu za upigaji mabomu uliopo sasa ambazo zinaleta maafa na zenye kutatiza, kwa kubadili mbinu hizo tunaweza kupata ufumbuzi...''
Amesisitiza kuwa njia pekee ya kuonesha uaminifu ni kuacha mashambulizi ya nga, vinginevyo amesema mazungumzo mengine yatakuwa hayana msingi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728