Dar es Salaam. Mvua kubwa isiyotabirika inatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini, maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba; pia katika ukanda wa Kaskazini Mashariki kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Tanga. Watu wasiojulikana wamevamia nyumba ya dereva wa bodaboda, Omari Shaaban (32) na kumuua kisha kuichoma moto, katika tukio linalohusishwa na visa na wivu wa mapenzi.
Dar es Salaam. Siku za wasafirishaji na wauzaji wa dawa za kulevya kwenda China sasa zinahesabika baada ya Jeshi la Polisi na kitengo chake cha Dawa za Kulevya kubaini majina ya vigogo wanaofanya shughuli hiyo na kusema imeanza kuwashughulikia kimyakimya.
HALI ya tafrani ilizuka jijini Dar es Salaam jana, baina ya Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa na
askari wa Jeshi la Polisi.
IKIWA imebaki miezi 10 kufikia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Askofu Mkuu
wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo,
amewataka Watanzania walio masikini kuungana ili kuwang’oa madarakani
viongozi matajiri wasiojali maslahi ya taifa.
MBIO za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimechukua sura mpya
baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kutangaza
rasmi nia ya kugombea urais mwaka 2015.
Wananchi wa Indonesia wameanza kuadhimisha mwaka wa kumi tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha mawimbi makubwa katika bahari ya Hindi, tsunami na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watu laki mbili na elfu ishirini katika eneo kubwa.
Kampuni ya Sony Pictures imesema kuwa sinema yenye utata ya ucheshi kuhusu namna ya kumuuwa kiongozi wa Korea Kaskazini, imewekwa katika mitandao Nchini Marekani.
Kocha wa Timu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kwa sasa hawana nafasi ya kumsaini mchezaji Lionel Messi kwa kuwa hakuna Fedha ya kutosha kumsajili mchezaji huyo .
Nchini Tanzania mtikisiko wa matokeo ya kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow umeendelea baada ya Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yake. Maswi anakuwa kiongozi wa tatu wa ngazi ya juu kukumbwa na upepo huo akitanguliwa na Mwanasheria mkuu wa serikali ambaye alijiuzulu mwenyewe na Waziri wa Ardhi aliyetimuliwa kazi hadharani na Rais Jakaya Kikwete. Licha ya kuondoka kwa viongozi hao bado baadhi ya wananchi na vyama vya upinzani wameendelea kulalamika kuwa juhudi za kutekeleza maazimio ya Bunge ni ndogo. Kuhusiana na hilo Baruan Muhuza wa BBC alizungumza na Neville Meena, katibu wa Jukwaa la wahariri Tanzania.
Uongozi wa Timu ya Manchester United umesema upo tayari kutoa paundi milioni 120 kwaajili ya kumsajili winga Gareth Balle mwenye umri wa miaka 25 kwa mwezi januari kutoka klabu ya Real Madrid , winga ambaye ni miongoni mwa wachezaji ghali zaidi ulimwenguni.