28 Januari 2015
FAHAMU MTANDAO WA SIMU
BUNGE
Ni siku nyingine katika wiki, bunge linaendelea leo kwa siku ya tatu tangu lianze wiki hii. Tutajuzana hapa kinachoendelea na ratiba ya leo itakua kama ifuatavyo.
Baadhi ya vijana wanaochukua mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Serikali imesitisha mafunzo ya JKT kwa mwaka huu. Kwa hiyo wale vijana waliokua wanategemea kuanza mafunzo hayo mwezi wa pili (tano) mwaka huu, mafunzo hayo hayatakuwepo tena.
Wahitimu mafunzo ya awali ya kijeshi kenye kambi ya JKT Ruvu kikosi cha singe wakiwa katika maonyesho ya kivita kwenye sherehe za kuhitimu mafunzo hayo
Sababu ya kusitisha mafunzo hayo ni ukata unaoikabili serikali.
Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Kikosi cha Ruvu, Kibaha, mkoani Pwani kwa mujibu wa sheria wakionyesha umahiri wao wa kuruka moto
27 Januari 2015
AMKA
MBINU ZA BIASHARA 1
SIRI YA UTAJIRI
JIBU LA KWA NINI WATU WENGINE NI MASIKINI NA WENGINE NI MATAJIRI
Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Jee ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida. Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila wanayo wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na huendelea kuificha. Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate manufaa kwa kununua kitabu hiki nimeamua kuiweka siri hii wazi:-
SHIDA YA UMEME KARIBUNI KWISHA
Dar es Salaam
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema halitaongeza mkataba na Kampuni ya kufua umeme ya Agreeko na Symbion kutokana na kukamilika kwa asilimia 72 mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kinyerezi 1.
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema halitaongeza mkataba na Kampuni ya kufua umeme ya Agreeko na Symbion kutokana na kukamilika kwa asilimia 72 mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kinyerezi 1.
26 Januari 2015
SOMA UTAPE MAARIFA
Nakukumbusha
SOMA HAPA USIJE KUFA KWA UZEMBE
Jumuiya ya madaktari wa Marekani imetoa majibu ya vyanzo vya cancer:-
1.Usinywe chai kwenye vikombe vya plastic.
2.Usile chochote chenye moto kilicho ndani ya mfuko wa plastic, mfano; chipsi.
3.Usipashe chakula kwenye microwave kwa kutumia chombo cha plastic.
KUMBUKA plastic ikikutana na joto inatoa kemikali inayosababisha aina 52 za cancer.
Kwahiyo Wafahamishe wote uwapendao ili waepukane na madhara haya.
Share kuwatahadharisha wenzako
SOMA HAPA USIJE KUFA KWA UZEMBE
Jumuiya ya madaktari wa Marekani imetoa majibu ya vyanzo vya cancer:-
1.Usinywe chai kwenye vikombe vya plastic.
2.Usile chochote chenye moto kilicho ndani ya mfuko wa plastic, mfano; chipsi.
3.Usipashe chakula kwenye microwave kwa kutumia chombo cha plastic.
KUMBUKA plastic ikikutana na joto inatoa kemikali inayosababisha aina 52 za cancer.
Kwahiyo Wafahamishe wote uwapendao ili waepukane na madhara haya.
Share kuwatahadharisha wenzako
De Jong eager to make Newcastle impact
Newcastle United travel to Hull City on Saturday boosted by the news that attacking midfielder Siem de Jong is close to making a first-team return for the Magpies, who on Monday confirmed that John Carver has been appointed head coach until the end of the season.
CHELSEA Vs MAN CITY
The encounter between Chelsea and Manchester City this weekend promises to be a fascinating contest between the two best teams in the Barclays Premier League. As we look forward to the showdown at Stamford Bridge, every day this week premierleague.com will be taking a closer look at the main protagonists in this top-of-the-table duel.
NCCR-Mageuzi wataka Rugemalira, Tibaijuka, Chenge wafikishwe mahakamani
Dar es Salaam. Chama cha NCCR-Magezi kimesema, vigogo wote waliohusika kutoa na kupokea mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow wafikishwe mahakamani akiwamo Mkurugenzi wa VIP Engineering Ltd, James Rugemalira .
Zitto: Escrow ni zaidi ya Muhongo
SIKU moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kutangaza kujiuzulu kutokana na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema suala hilo bado ni bichi.
Dawa hizi ni hatari kwa binadamu – TFDA
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA), imeziondoa sokoni na kuzifutia usajili aina tano za dawa zinazotumiwa na binadamu baada ya kugundulika kuwa zina madhara katika mwili wa binadamu.
Butiku ahamasisha kura ya hapana Katiba Mpya
WAJUMBE wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wamewataka Watanzania kuikataa Katiba inayopendekezwa kwa kuwa haikuzingatia masilahi ya Watanzania.
21 Januari 2015
Wasiwasi watanda Kinshasa
18 Januari 2015
3,052 Baptized and 200 Pastors Ordained in Dominican Republic A historic Sabbath caps the Adventist Church’s Ten Days of Prayer.
Thousands of people packed a stadium in the Dominican Republic’s capital on Sabbath to celebrate 3,052 baptisms and the historic ordination of more than 200 pastors at the close of a worldwide Ten Days of Prayer initiative by the Seventh-day Adventist Church.
The worship service at Santo Domingo’s El Palacio de Los Deportes stadium, transmitted live online and via radio and television, was attended by the Adventist Church’s 29 top leaders, including General Conference president Ted N.C. Wilson, who preached the sermon.
Hivi kweli bado tuko makini na kura ya maoni aprili 30?
Zikiwa zimesalia siku 42 kufika tarehe 1 Machi 2015, tarehe ambayo kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Kura ya Maoni ndiyo siku ambayo Asasi za Kiraia baada ya kupewa ruhusa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitaanza kutoa elimu ya uraia juu ya Katiba Inayopendekezwa.
Ngeleja agoma kung’oka
MWENYEKITI wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja, ameendelea kushikilia msimamo wake kutojiuzulu nafasi yake hiyo kama ilivyoelekezwa katika maazimio nane ya Bunge.
Vituko vya mwakilishi wa Rais Kikwete
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, ambaye ni mwakilishi wa Rais Jakaya Kikwete mkoani hapa, amebuni aina mpya ya ulinzi wake binafsi pamoja na msafara wa magari unaoambatana naye anapokuwa katika ziara zake za kikazi.
Lembeli: Tutasafisha Wizara ya Ardhi
IKIWA ni takriban wiki tatu tangu Rais Jakaya Kikwete amuondoe kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imesema itahakikisha viongozi wanaofanya vitendo vya kifisadi katika wizara hiyo wanaondolewa.
Escrow yauma vigogo BoT, TRA
MKURUGENZI wa Fedha wa Benki Kuu, Julius Angello, Meneja wa Misamaha ya Kodi wa TRA, Kyabukoba Mutabingwa na Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Urassa wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kupokea rushwa ya zaidi ya Sh bilioni mbili kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
EPL KUMECHAFUKA MAN CITY AUWAWA 2 ARSENAL WAZIDI KUTAKATA
MATOKEO YA KIDATO CHA PILI MWAKA 2015
17 Januari 2015
09 Januari 2015
Pinda akana kulialia
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema yeye si kiongozi wa kulialia jambo ambalo linamfanya ashindwe kutoa maamuzi mbalimbali ya Serikali kama watu wengi wanavyodai.
Jaji akumbusha machungu kifo cha Daudi Mwangosi
MWENYEKITI wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) aliyemaliza muda wake, Jaji Amir Manento, ameonyesha kutofurahishwa na Serikali kushindwa kutekeleza ripoti iliyotolewa na tume hiyo kuhusu mauaji ya mwandishi wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.
Panya Road wafurika mahabusu Dar
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limeendelea na kamatakamata ya vijana wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha na uporaji, walio maarufu kwa jina la Panya Road.
Raia wa Kuwait akamatwa na kenge 149
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia raia wa Kuwait, Hussein Mansour (34), baada ya kukamatwa Uwanja wa Ndenge wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa kuamkia jana akijaribu kusafirisha kenge hai 149.
08 Januari 2015
Baba amtupa mwanawe ndani ya maji
Mwanaume mmoja amefikishwa
mahakamani kwa kosa la mauaji baada ya polisi kudai kuwa alimtupa mtoto
wake mwenye umri wa miaka 5 kutoka juu ya daraja mjini St Petersburg.
Afisa
wa polisi alisema alijionea tukio hilo la kushangaza baada kumwandama
John Jonchuck Jr, mwenye umri wa miaka 25, baada ya kuona akiendesha
gari lake kwa kasi, alisema afisaa mkuu wa polisi Anthony Holloway.Mtoto huyo aliyetupwa ndani ya maji yenye kina cha mita 18 alipatikana akiwa amefariki saa moja baadaye.
Polisi hawana uhakika ikiwa mtoto huyo alifariki kabla ya kutupwa ndani ya maji lakini uchunguzi bado unafanywa.
Bwana Jonchuck alikamatwa dakika 30 baadaye na alitarajiwa kufikishwa mahakamani Alhamisi.
Holloway alisema afisaa mmoja wa polisi ambaye alikuwa likizoni alishtushwa na gari lililompita kwa kasi likiwa likendeshwa kwa kilomita 161 kwa saa na bwana Jonchuck..
Afisaa huyo ambaye hakutambuliwa aliendesha gari lake kwa kasi na kumfuata Jonchuck ambaye alisimamisha gari lake ghafla.
Jonchuck aliondoka kwenye gari lake na kumkaribia polisi na muda si muda alikwenda upande mwingine wa gari na kumchukua mwanawe, kumkumbatia kwa muda. Polisi alisema alisikia mtoto huyo akipiga mayowe lakini hakumbuki vyema kwani muda mfupi baadaye babake mtoto huyo alimtupa ndani ya maji umbali wa kilomita 2.4 kutoka juu ya daraja hilo.
''Baada ya kitendo chake mshukiwa alitoroka,'' alisema afisaa huyo wa polisi.
Nimekuwa nikiwashika wahalifu kwa miaka 29, lakini sijawahi kujionea kitu kama hiki sina habari kabisa alichokuwa anakitafakari mshukiwa huyo.
Bwana Jonchuck, anayeishi na babake alikuwa ameruhusiwa na mahakama kuishi na mwanawe baada ya kukosana na mama ya mtoto huyo. Aliwahi kushitakiwa kwa kosa la kumchapa mkewe pamoja na kuendesha gari lake akiwa mlevi mwaka 2013.
Fernando Torres arejea kwa kishindo
Fernando Torres arejesha ushindi
katika klabu yake ya Atletico Madrid kwa kuwabamiza Real Madrid 2-0
katika michuano ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey.
Chelsea yamtaka Messi kwa pauni milioni 200
Lionel Messi ameambiwa kwamba kuna mkataba wa miaka sita kutoka kwa kilabu ya Chelsea unaomngojea.
Duru
za karibu na mchezaji huyo wa Barcelona zinaarifu kuwa Chelsea imeweka
wazi kwamba iko tayari kutoa kitita cha pauni millioni 200 kumnunua
nyota huyo.Vilevile The Blues imedaiwa kwamba iko tayari kulipa mahitaji yake ya mshahara ambayo huenda yakaongeza kiwango hicho mara mbili.
Mnamo mwezi Novemba kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikana habari zinazoihusisha kilabu hiyo na Messi,lakini katika kilabu ya Barcelona kumekuwa na mgogoro tangu wakati huo na ripoti kutoka Uhispania zinasema kuwa mchezaji huyo amekuwa akizozana na muajiri wake Luis Enrique.
Inadiwa kuwa Mesi hakushiriki katika mazoezi ya siku ya jumatatu huku Enrique akishindwa kukana mgogoro uliopo kati yake na Messi.
07 Januari 2015
Mwanamume mweye jinsi mbili asimulia maisha yake
BBC, Uingereza. Mwanamume mwenye jinsi mbili, amezungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na kusema kama wazazi wake wangemshauri kuhusu hali hiyo, asingeogopa kujitambulisha ulimwenguni.
Ngumi, mabomu uapishaji wenyeviti wa mitaa
ENEO la Riverside Ubungo jijini Dar es Salaam, jana liligeuka uwanja wa mapambano baada ya polisi kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi ili kunusuru hafla ya kuapishwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Wilaya ya Kinondoni.
ACT-Tanzania vipande vipande
I wazi sasa hali ya mambo ndani ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) si shwari kutokana na chama hicho kuwa vipande vipande.
Kashfa ya Escrow yamng’oa Chenge rasmi
WAKATI Watanzania wakisubiri hatima ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye Rais Jakaya Kikwete alisema anamuweka kiporo kutokana na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge, ametangaza rasmi kuachia nafasi hiyo.
05 Januari 2015
Watoto wazaliwa wameungana
MKAZI wa Kata ya Buhare Manispaa ya Musoma, Helena Paulo (21), amejifungua watoto pacha walioungana sehemu za kifuani na tumboni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
Mila zazua mtafaruku makaburini
Matafaruku mkubwa umetokea baada ya ndugu wa marehemu, kumpasua tumbo ndugu yao na kumuwekea kifaranga cha kuku wakati akizikwa.
AG MASAJU: Nitaanza na mikataba ya gesi
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, amesema anataka muda zaidi ili aweze kuzungumzia suala la Kampuni ya Kufua Umeme Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na mikataba ya gesi ambayo imekuwa ikitakiwa kuwekwa wazi.
Korea Kazkazini yaionya Marekani
Korea kazkazini imeonya kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi yake ni kitendo cha uadui ambacho hakitafanikiwa.
Yanga yatinga robo fainali Mapinduzi Cup
TIMU ya Yanga jana ilitinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kuichapa Polisi ya humo mabao 4-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan.
04 Januari 2015
Sitta apinga magari ya Tanzania kuzuiwa Kenya
ARUSHA
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ameshtushwa na hatua ya Serikali ya Kenya kuyazuia magari yenye namba za usajili za Tanzania kuingia katika eneo la maegesho ya magari katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata na kuweka wazi kuwa ni hatua isiyokubalika.
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ameshtushwa na hatua ya Serikali ya Kenya kuyazuia magari yenye namba za usajili za Tanzania kuingia katika eneo la maegesho ya magari katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata na kuweka wazi kuwa ni hatua isiyokubalika.
Membe, January wahofia urais
Kimwanga na Asifiwe George, Dar es Salaam
MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bernard Membe na January Makamba ambao wametangazi nia ya kugombea urais mwaka huu, wameanza kuonesha hofu kuhusu nafasi hiyo ya juu nchini.
MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bernard Membe na January Makamba ambao wametangazi nia ya kugombea urais mwaka huu, wameanza kuonesha hofu kuhusu nafasi hiyo ya juu nchini.
Mwili wa marehemu wazikwa na kuku tumboni
Shinyanga
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa Benadetha Steven (35), aliyefariki dunia juzi umefanyiwa matambiko ya kimila baada ya kupasuliwa na wembe ukiwa kaburini na kuingiziwa kuku ndani ya tumbo lake ikiwa ni ishara ya kuondoa mkosi.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa Benadetha Steven (35), aliyefariki dunia juzi umefanyiwa matambiko ya kimila baada ya kupasuliwa na wembe ukiwa kaburini na kuingiziwa kuku ndani ya tumbo lake ikiwa ni ishara ya kuondoa mkosi.
Escrow yazamisha watatu urais 2015
KASHFA ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, imewachafua viongozi watatu ambao walishaanza harakati za kuusaka urais kwa mwaka 2015.
Siri nzito uteuzi wa mawaziri
Dar es Salaam. Wakati wowote Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuipanga safu mpya ya Baraza la Mawaziri kwa kuteua waziri mwingine wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya kumwondoa aliyekuwepo, Profesa Anna Tibaijuka.
Atangaza kuuza figo kwa sh 90 mil
Mkazi wa Morogoro, Andrew Germanis Chimulimuli ametangaza kuingiza sokoni figo yake ambayo amesema anaiuza Sh90 milioni ili kukabiliana na ugumu wa maisha.
03 Januari 2015
IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dk.Mighanda Manyahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)