Matafaruku mkubwa umetokea baada ya ndugu wa marehemu, kumpasua tumbo ndugu yao na kumuwekea kifaranga cha kuku wakati akizikwa.
Tukio hilo limetokea mkoani Shinyanga, kaskazini magharibi mwa Tanzania, baada ya ndugu wa marehemu Bernadetha Steven kufungua jeneza wakati akizikwa na kumtumbukiza kifaranga tumboni.
Amon Meshack, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiishi na marehemu anasema baada ya mwili wa marehemu kufikishwa makaburini na wakati salama ya mazishi ikiendelea, alitokea kaka wa marehemu na kuingia katika kaburi na kukaa juu ya jeneza, pamoja na ndugu mwingine aliyekuwa ameshika kifaranga cha kuku, ghafla walifungua jeneza hilo na kuanza kumchanja ndugu yao pembeni ya kitovu huku wakikichinja kifaranga hicho na damu yake kunyunyuzia katika eneo hilo na hatimaye kukizamisha kifaranga cha kuku katika eneo hilo la tumbo.
Tukio hilo ambalo lilisitisha shughuli nzima ya maziko kwa muda linaelezwa kwamba ni sehemu ya mila za Wakurya, kabila ambalo ni la marehemu.
Siku moja kabla ya maziko hayo, baadhi ya ndugu wa marehemu walitishia kususia kushiriki mazishi, mpaka pale watakapomaliziwa kulipwa mahari iliyobakia, walidai kulipowa shilingi milioni moja, na kwamba kinyume na masharti wangeondoka na mwili wa ndugu yao, lakini hata hivyo waliambuliwa kulipwa shilingi laki moja tu.
Hali hiyo ilileta mtafaruku katika eneo hilo la makaburi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni