Fernando Torres arejesha ushindi
katika klabu yake ya Atletico Madrid kwa kuwabamiza Real Madrid 2-0
katika michuano ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey.
Mbele ya umati wa mashabiki 46,800 waliokuwa wakiishuhudia mechi hiyo ya aliyekuwa mchezaji mahiri wa timu za Liverpool na Chelsea, amerejea katika timu yake iliyomkuza na kumtambulisha kipaji chake, Atletico Madrid.
Raul Garcia,aliipatia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 58 akifunga kwa njia ya penalti, huku Jose Maria Gimenez akikamilisha ushindi wa Atletico kwa kufunga bao kwa njia ya kichwa katika dakika ya 76 ya mchezo.
Torres mwenye miaka 30 alibadilishwa katika dakika ya 59. Mchezaji aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka katika timu ya Italia ya AC Milan wiki iliyopita, ndiye aliyeongoza kwa ufungaji katika timu ya Atletico kwa misimu mitano kabla hajatia mguu Liverpool mwaka 2007.
Mashabiki wapatao 45,000 waliishuhudia mechi iliyopigwa katika uwanja wa Vicente Calderon mnamo siku ya Jumapili wakati ambapo utambulisho wa Torres ulipofanyika na papo hapo jezi zenye jina lake zikaanza kuuzwa ambapo ndani ya saa 24, ziliuzwa jezi 2,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni