Mwanaume mmoja amefikishwa
mahakamani kwa kosa la mauaji baada ya polisi kudai kuwa alimtupa mtoto
wake mwenye umri wa miaka 5 kutoka juu ya daraja mjini St Petersburg.
Afisa
wa polisi alisema alijionea tukio hilo la kushangaza baada kumwandama
John Jonchuck Jr, mwenye umri wa miaka 25, baada ya kuona akiendesha
gari lake kwa kasi, alisema afisaa mkuu wa polisi Anthony Holloway.Mtoto huyo aliyetupwa ndani ya maji yenye kina cha mita 18 alipatikana akiwa amefariki saa moja baadaye.
Polisi hawana uhakika ikiwa mtoto huyo alifariki kabla ya kutupwa ndani ya maji lakini uchunguzi bado unafanywa.
Bwana Jonchuck alikamatwa dakika 30 baadaye na alitarajiwa kufikishwa mahakamani Alhamisi.
Holloway alisema afisaa mmoja wa polisi ambaye alikuwa likizoni alishtushwa na gari lililompita kwa kasi likiwa likendeshwa kwa kilomita 161 kwa saa na bwana Jonchuck..
Afisaa huyo ambaye hakutambuliwa aliendesha gari lake kwa kasi na kumfuata Jonchuck ambaye alisimamisha gari lake ghafla.
Jonchuck aliondoka kwenye gari lake na kumkaribia polisi na muda si muda alikwenda upande mwingine wa gari na kumchukua mwanawe, kumkumbatia kwa muda. Polisi alisema alisikia mtoto huyo akipiga mayowe lakini hakumbuki vyema kwani muda mfupi baadaye babake mtoto huyo alimtupa ndani ya maji umbali wa kilomita 2.4 kutoka juu ya daraja hilo.
''Baada ya kitendo chake mshukiwa alitoroka,'' alisema afisaa huyo wa polisi.
Nimekuwa nikiwashika wahalifu kwa miaka 29, lakini sijawahi kujionea kitu kama hiki sina habari kabisa alichokuwa anakitafakari mshukiwa huyo.
Bwana Jonchuck, anayeishi na babake alikuwa ameruhusiwa na mahakama kuishi na mwanawe baada ya kukosana na mama ya mtoto huyo. Aliwahi kushitakiwa kwa kosa la kumchapa mkewe pamoja na kuendesha gari lake akiwa mlevi mwaka 2013.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni