Lionel Messi ameambiwa kwamba kuna mkataba wa miaka sita kutoka kwa kilabu ya Chelsea unaomngojea.
Duru
za karibu na mchezaji huyo wa Barcelona zinaarifu kuwa Chelsea imeweka
wazi kwamba iko tayari kutoa kitita cha pauni millioni 200 kumnunua
nyota huyo.Vilevile The Blues imedaiwa kwamba iko tayari kulipa mahitaji yake ya mshahara ambayo huenda yakaongeza kiwango hicho mara mbili.
Mnamo mwezi Novemba kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikana habari zinazoihusisha kilabu hiyo na Messi,lakini katika kilabu ya Barcelona kumekuwa na mgogoro tangu wakati huo na ripoti kutoka Uhispania zinasema kuwa mchezaji huyo amekuwa akizozana na muajiri wake Luis Enrique.
Inadiwa kuwa Mesi hakushiriki katika mazoezi ya siku ya jumatatu huku Enrique akishindwa kukana mgogoro uliopo kati yake na Messi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni