24 Septemba 2014

Kili Music Tour yafanya kweli Tanga


Tamasha la Kili Music Tour linalodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager limeacha gumzo kubwa Tanga huku wasanii walioshiriki ziara ya muziki ya Kilimanjaro, inayotia nanga wiki hii katika viwanja vya Leaders kwa nyakati tofauti wamekiri kwamba kila mmoja kwa njia yake amejifunza makubwa katika ziara hiyo ambayo wengi wameitaja kuwa ni ziara namba moja kwa ubora

Wakiongea na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mara baada ya kushuka jukwaani wasanii hao waliisifu ziara hiyo kwanza kwa kuwa ni ziara inayowaweka wasanii kwenye hadhi lakini pia ni ziara ambayo ina mpangilio wa kueleweka.

Waliongea katika tamasha kubwa lililofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani ambako maelfu ya mashabiki walijitokeza na kupata burudani ya aina yake iliyodumu kwa zaidi ya saa saba huku ikiwa na msisimko kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Kwa upande wake Omary Nyembo au Ommy Dimpoz kama alivyozoeleka kuitwa na mashabiki wake, amesema Kili ni ziara iliyomuweka karibu na mashabiki wake wa kipato cha chini baada ya kuwa ni ziara yenye viingilio vya chini iliyohusisha wasanii wakubwa nchini.

Rich Mavoko, nyota wa wimbo unaotamba sasa hivi wa 'Roho Yangu' aliwaambia waandishi wa habari kwamba mwisho wa ziara hiyo ndiyo mwanzo wa kujipanga kwake kwa ajili ya ziara ya mwakani na ameahidi kurudi vingine huku akiwa ameongeza nguvu katika utendaji wake jukwaani.

Joseph Haule au Profesa Jay aliisifia ziara hiyo na wadhamini wake, Kilimanjaro Premium Lager kwa kuandaa ziara ya kizalendo ambayo imekuwa ikizunguka nchi nzima kuwanadi wasanii wa nyumbani na kuwakutanisha na mashabiki wao bila kuangalia faida, bali kuhakikisha muziki nwa Kitanzania unafika katika kilele cha mafanikio.

Kundi la muziki la Weusi lililo na wanamuziki watatu; Joh Makini, Nikki wa Pili na G Nako, wakiwakilishwa na msemaji wao Nikki wa Pili kwa upande wao waliishukuru kampuni ya Bia Tanzania kwa kuwapa nafasi ya kupanda katika majukwaa ya mikoa yote Tanzania ambako wamefanikiwa kuwaonesha mashabiki wao uwezo wao kikazi lakini pia wamejenga mahusiano na wadau.

Wasanii walioshiriki tamasha hilo ni pamoja na Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Ben Paul, Khadija Kopa, Mzee Yusuph, Profesa Jay na Weusi.

Kili Music Tour inaratibiwa na East Africa Radio na Tv, Executive Solutions, Integrated Communications, Aggrey & Clifford na Aim Group.Baada ya kuzunguka mikoa tisa, Jumamosi ijayo ni zamu ya Dar es Salaam ambako ziara hii itahitimishwa kwa kishindo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728