23 Septemba 2014

Wasira: Urais si mama mkwe

Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wasira amesema hana sababu ya kuona haya kutangaza kuutaka urais kwa kuwa urais si ukwe ila anasubiri wakati mwafaka. Wasira alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili mjini Dodoma. “Watakaposema ruksa, nitasema na wala kugombea urais si suala la kuonea haya. Ni kutoa huduma kwa Watanzania. Unalionea haya la nini? Kwani kugombea urais ni ukwe?” alihoji Wasira na kuendelea; “Urais ni mama mkwe wako, hapana. Wakati ukifika nitasema tu. Na mradi kuna wananchi wanasemasema na wananitia moyo, ukifika wakati nitasema.” Hata hivyo, waziri huyo ameonya kuwa endapo urais utachezewa kwa kuingia mtu ambaye si mwadilifu, biashara atakayoifanya Ikulu itakuwa ni kuuza haki za watu. Alisema hawezi kufahamu nani atashinda katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani, lakini lazima rais awe mtu mwenye sifa za kushika nafasi hiyo.
“Mimi siwezi kufahamu ni nani ataongoza Tanzania, lakini ninaweza kusema sifa.” Alisema Wassira na kutaja sifa hizo kuwa ni pamoja na kuwa Mtanzania kwa sababu haiwezekani kuagiza mtu kutoka nje ya nchi kuja kuwania nafasi hiyo. Aliongeza; “Rais pia anatakiwa kuwa mzalendo anayeipenda nchi yake na adhihirishe mapenzi yake, awe na uwezo wa kuongoza na pia ame-prove (amedhihirisha) uwezo wake huo wa kuongoza.” Sifa nyingine ya urais, aliitaja kuwa ni mgombea kuwa mtu aliyewahi kuongoza taasisi nyingine na kuwaridhisha Watanzania kuwa aliongoza vizuri. “Lakini pia rais lazima awe mwadilifu maana unalinda haki za watu. Baba wa Taifa aliwahi kusema Ikulu kuna biashara gani, lakini kuna biashara ya nguvu tu. Unaweza kuuza haki za hao watu,” alisema na kuongeza; “Maana chakuuza pale hakuna. Mimi nafanya pale. Mimi naona watu wanamwagilia maua tu lakini kuna power (nguvu), kama wewe unapenda hela zaidi kuliko watu waliokuweka pale basi wewe utakuwa kazi yako ni kuuza haki zao.” Alisema sifa hizo ni za msingi na wala si ngumu na kama mtu hana, hana tu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728