24 Septemba 2014
Chui Buka amuua mwanafunzi India
Chui Buka au 'Tiger', amemshambulia na kumuua mwanafunzi nchini India katika hifadhi ya wanyamapori ya Delhi. Msimamizi wa mbuga hiyo Riaz Khan amesema mvulana huyo alikuwa amevuka ua unaomfungia Chui huyo hatari.
Ripoti za mwanzoni zilimtaja mvulana huyo kuwa mwanafunzi. Picha za televisheni zilionyesha mwanafunzi huyo akiwa amejibana ukutani akijaribu kujikinga huku Chui huyo akiwa amesimama karibu naye.
Kwa mujibu wa mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, mvulana huyo alikuwa amejiegemeza kwenye ua huo uliokuwa mfupi sana.
''Mwendo wa saa saba unusu tulikuwa katika eneo lililo na wanyama wengine tuliposikia mayowe," Himanshu aliyeshuhudia tukio hilo aliambia CNN.
''Nilikimbia nikielekea eneo ambalo Chui huyo alikuwa amefungiwa, nikapata Chui Buka mweupe amemuuma mwanafunzi huyo shingoni huku akilia na kufurukuta kwa uchungu.
Watoto wengine walijaribu kumrushia chui huyo vijiti na mawe. Mvulana huyo aliumia kwa zaidi ya dakika kumi bila yeyote kumsaidia" Himanshu alisema polisi walifika ''haraka sana" lakini hawangeweza kumwokoa kijana huyo.
Kituo cha habari cha Reuters kilimnukuu mwelekezi wa hifadhi ya kitaifa ya wanyamapori ambayo inasimamia mbuga ya Delhi bw. Amitabh Agnihotri, akisema ameshtuliwa sana na kisa hicho.
''Bado sina uhakika kama kijana huyo aliruka ndani ya mbuga ama aliteleza kibahati mbaya," aliongeza.
Mwili huo umepelekwa kufanyiwa upasuaji ili kuthibitisha kilichotendeka huku polisi wakianzisha uchuguzi kuhusu tukio hilo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni