DEREVA wa pikipiki (bodaboda) Emanuel Kahemela aliyehukumiwa kifungo cha uangalizi kwa mwaka mmoja nje katika kesi ya kubaka kwa kuishi na binti (jina linahifadhiwa) mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mlamke ya Halmashuri ya Manispaa Iringa, amemtorosha tena.
Kahemela, alimtorosha binti huyo kwa kipindi cha miezi mitatu na kwenda kuishi naye kinyumba kabla ya kukamatwa na kuhukumiwa kifunguo hicho ambacho alikiuka.
Akizungumza na Tanzania Daima, Yusuph Mwimbage, alisema Kahemela alifunguliwa kesi ya kubaka na polisi yenye namba IR/RB/5156/2014, ambayo ilifunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa, ambako Hakimu John Mpitanjia alitoa hukumu hiyo.
Mwimbage, alisema baada ya hukumu hiyo Kihemela alirudi nyumbani kwa mlezi wa binti huyo Amina Mwimbage, ambako alifanya vurugu kisha kumtorosha tena binti huyo.
Alisema walipofuatilia mahakamani walibaini hukumu ilitolewa bila walezi wa binti huyo kuwepo hali inayozua shaka, kwa kuwa walipofuatilia walibaini kulikuwa na ujanja umefanyika kupunguza umri wa Kahemela, kutoka miaka 21 hadi 17.
Alisema ujanja huo ulifanywa kwa lengo la kumuepusha kijana huyo kuhukumiwa kama mtu mzima, kwa kuwa sheria inatambua umri wa mtu mzima unaanzia miaka 18.
“Sisi tunaomba ngazi za juu zilifuatilie suala hili maana tunaona haki inaminywa, binti yetu ameachishwa shule na kutoroshwa….hii si haki hata kidogo,” alisema.
29 Septemba 2014
Dereva bodaboda atuhumiwa kumtorosha mwanafunzi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni