16 Septemba 2014
SABATO YA WAGENI
Kanisa la waadventista wasabato External-Ubungo,Dar es salaam limeandaa sabato ya wageni itakayo fanyika siku ya jumamosi tarehe 4 mwezi wa kumi mwaka huu 2014. Wazee wakanisa na washiki wote wa External wanayo furaha kukualika,kuwaalika nyote kuhudhulia katika siku hiyo kuu. kutakuwa na mafundisho makuu ya neno la Mungu,programu mbalimbali za watoto,vijana. Siku hiyo tutakaa pamoja wote tukijumuika kwa chakula cha kimwili na kiroho pia utakuwepo muda au kipindi kizuri cha kuwatunuku zawadi kwa wageni wote watakao hudhulia siku hiyo. Siku hii kuu watu wote mnaalikwa kwa kila kabila,lugha na jamaa alika na wenzako wote tujumuike kwa pamoja tupate mibaraka.Mungu akubariki sana unapopanga kutokukosa mibaraka hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni