23 Septemba 2014
Man U hoi, Chelsea na Man citty washindwa kutambiana
London, England. Leicester City ilitoka nyuma kwa mabao 3-1 na kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana.
United walionekana kama wangeibuka na ushindi wakati Robin van Persie alipofunga bao la mapema kabla ya Angel Di Maria kufunga la pili, lakini bao la kichwa la Leonardo Ulloa lilifanya matokeo kuwa 2-1 kabla ya Ander Herrera kufunga la tatu kwa United.
Leicester walirudi uwanjani kwa kasi na kupata penalti iliyofungwa na David Nugent na Esteban Cambiasso alisawazisha bao la tatu, wakati Jamie Vardy akifunga la nne kabla ya Ulloa kufunga la tano.
Ikiwatumia washambuliaji watatu, Radamel Falcao, Wayne Rooney na Robin van Persie, United ilishindwa kucheza vizuri katika kipindi cha pili na kuiruhusu Leicister kumiliki mpira walivyotaka.
Bao la Andre Schurrle la kipindi cha pili lilisawazishwa na Frank Lampard na kufanya mchezo kati ya Manchester City na Chelsea kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Vijana wa kocha Jose Mourinho walilazimisha sare hiyo ugenini katika Uwanja wa Etihad na kufikisha pointi 13 kileleni ikiwa na michezo mitano iliyocheza.
Katika mchezo huo, beki wa pembeni wa City, Pablo Zabaleta alitolewa kwa kadi ya pili ya njano kutokana na kumchezea vibaya Diego Costa kipindi cha pili.
Mchezo huo ulionyesha kuwa ungekuwa na kadi nyekundu baada ya wachezaji saba kuonyeshwa kadi za njano katika kipindi cha kwanza. Kwa matokeo hayo, Chelsea imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo ikiwa na tofauti ya pointi tatu, ikifuatiwa na Southamptom wenye pointi 10
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni