Duniani kuna afua mbili. Kufa au kupona.
Jamii nyingi hutofautiana jinsi wanavyomkaribisha mwana wao humu duniani na pia jinsi wanavyopuaga anatangulia mbele ya haki.
Katika jamii nyingi duniani, kuna tamaduni tofauti za kuomboleza,kuadhimisha, na kuwazika wapendwa wao.
Jamii moja inayoonesha mbinu za kipekee za kuomboleza na ya kupigiwa mfano ni ile ya Dani, iliyoko Magharibi mwa Papua New Guinea.
Tabaka hilo huwa linaomboleza wapendwa wao kwa kujikata vidole vyao, kama dhihirisho ya kuwa kweli ulikuwa unampenda yule aliyeaga dunia !
Tamaduni hiyo ambayo inaonekana ya kutisha imekita mizizi sana miongoni mwao na si ajabu unapotembeatembea kijijini utashangaa kuwaona watu waliokatwa viganja vyao vikaisha.
Hilo likiwa dhirisho kuwa amefiwa na wapendwa wake.
Wakaazi hao wa bonde la Baliem wamekuwa wakifuata tamaduni hiyo kwa miaka na mikaka na hivyo sio jambo ambalo linawezatoweka kwa haraka.
Mtindo huu hufanyika kwa yeyote ule mwenye uhusiano na marehemu, wakiwajumuisha wazee, wanawake na hata watoto.
Utamaduni huo huanza kwa ibada kwa minajili ya kufukuza mapepo ya marehemu, na pia kama njia ya kutumia maumivu ya kimwili kuonyesha huzini na mateso ya kufiwa.
Vidole vyao hufungwa kwa kamba, kisha kukatwa na shoka, vipande vilivyokatwa huchomwa kwa moto na jivu huhifadhiwa.
Wakati mwengine vipande hivyo huzikwa pamoja na marehemu.
Vidole hukatwa hususan kuonyesha upendo kwa marehemu.
Kwa mfano, mume au mke hukatwa kidole na kukizika pamoja na maiti ya mume au mke wake, kama ishara ya upendo.
Haijabainika ni kidole kipi kinachopendelewa ama ishara ya mwili na roho kuunganishwa pamoja milele.
Idadi ya vidole vinavyokatwa ni shara ya wale waliofiwa na waliopendwa katika jamii.
Jitihada zimeanza kufanywa ilikusimamisha matambiko ambayo yanahusisha utamaduni huu ambao madhara yake yanabainika katika jimbo lote wakaoishi jamii hii.
Je tamaduni zako zinakushurutisha kufanya nini ilikumuaga mpendwa wako ?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni