Baadhi ya watu hutanabahi wanapokuwa hawajapata usingizi wa kutosha,lakini ni wa kutosha kwa kiasi gani? Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani, unapendekeza kuwa jibu la swali hilo, hutegemeana na umri wako!
Ukosefu wa kawaida wa usingizi,unywaji wa pombe,ama vimiminka vyenye kuamsha hisia za mwili ,kama kahawa,vichechemua mwili,usihesabu kengele ya saa asubuhi yenye kuashiria muda wa kuamka na jua lasiku,hivi vyote vinaingilia utaratibu wa mwili kwa kawaida hujulikana kama saa asili.
Kitengo cha utafiti kutoka nchini Marekani kijulikanancho kama US National Sleep Foundation (NSF), kilichoko Arlington, huko Virginia, kinaeleza kuwa maisha ya mtu mzima huonesha mahitaji ya usingizi,lakini kuna maelezo zaidi kulingana na umri ulionao.
Watoto wachanga wenye umri kati ya 0 hadi miezi mitatu wao wanapaswa kulala kati ya saa 14 hadi 17 kila siku,lakini hata akilala muda wa saa 11 hadi 13 inaweza kuwa sawa.lakini inashauriwa kulala zaidi saa 19.
Watoto wenye umri wa miezi 4 hadi 11 muda wa kulala kwa watoto wa umri huo unashauriwa kuwa kati ya saa kumi na mbili hadi kumi na tano,laikini walau alale kwa saa kumi inatosha sana,na si sawa tena haishauriwi mtoto alale kwa zaidi ya saa kumi na nane.
Walio na umri wa mwaka mmoja hadi miaka miwili wao wanashauriwa kulala kati ya saa kumi na moja hadi kumi na nne ,lakini muda uliokubalika ni saa tisa hadi kumi na sita.Wale wanaotarajiwa kuanza shule wenye umri wa miaka mitatu hadi mitano, watalaamu wanashauri walale si chini ya saa nane ama zaidi ya saa kumi na nne .Wanafunzi wa shule za awali wenye umri wa miaka sita hadi kumi na sita wao wanashauriwa kulala kwa saa tisa hadi kumi na moja,na kiafya endapo watalala chini ya saa saba ama zaidi ya saa kumi na mbili haishauriwi kiafya.Watoto wanaopevuka wenye umri wa miaka kumi nan ne hadi kumi na saba saa wanazo shauriwa kulala ni saa nane hadi kumi. Lakini NSF wanaonya wasilale zaidi ya saa kumi na moja ama chini ya saa saba.Wenye umri wa kati ,nazungumzia miaka kumi na nane hadi ishirini na tano ,inashauriwa watu wa umri wa kati walale saa saba hadi tisa ,lakini isiwe chini ya saa sita na si zaidi ya saa kumi na moja.Watu wazima wenye umri wa miaka ishirini na sita hadi sitini nan ne ni sawa na wale waumri wa kati hapo juu.Na wale wenye umri wa miaka sitini na tano na zaidi kwa afya zaidi, muda wa kulala ni saa saba hadi nane kwa siku lakini si chini ya saa tano ama zaidi ya saa tisa.
Wataalamu wa usingizi NSF wamechapisha orodha ya maelezo ya kuboresha kiwango cha usingizi zaidi.
Kwanza na zaidi ya hapo wanasema kwamba usingizi ama kulala kunapaswa kupewa kipaumbele,lakini wataalamu hao wanasema kwamba dondoo hizi zifuatazo nazo ni muhimu kwa afya na usingizi wako.
Zingatia muda wako wa kulala,hata mwishoni mwa juma.Buni namna na mbinu za kupumzika vyema zaidi iwe kama ibada iso badilika badilika. Fanya mazoezi kila sikuHakiki masula ya kiwango cha joto chumbani nah ii ikiwa ni pamoja na sauti pamoja na taa za chumbani.Lala katika godoro linalokupa raha na starehe na hata mito nayo pia ikupe pumziko .Epuka vinywaji vizuiavyo usingizi kama kahawa na pombe.Zima vifaa vya umeme.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni