Jana wakati mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema , akichangia hoja Bungeni nakudai kuwa mawaziri wengi hawana ubunifu nakumrushia “bomu” Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa anazunguka nje ya nchi na msichana kwa madai ya kutangaza utalii.
Lema alisema;
“Angalia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alikwenda kutangaza utalii nje ya nchi akiwa ameongozana na (mwigizaji maarufu wa filamu wa hapa Bongo) Anti Ezekiel,” alisema na kuongeza kuwa waziri huyo hashindi ofisini kwa kisingizio cha kutangaza utalii.
Picha za wawili hawa wakiwa nchini Marekani wakitangaza utalii zilisambaa sana mtandaoni mwaka jana na kizua stori nyingi juu kile kilichofanyika.
Picha : Waziri Nyalandu akiwana Aunty Ezekiel pamoja na DJ Luke (wakatikati) wakitangaza Utalii, New York, Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni