Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa hawana ushahidi wowote kuthibitisha madai kutoka kwa kundi la Islamic State kuwa mwanamke raia wa Marekani Kayla Mueller ambaye alikuwa akishikiliwa mateka na wanamgambo hao aliuawa kwenye mashambulizi ya ndege za kijeshi yaliyoendeshwa na Jordan nchini Syria.
Katika taarifa ya Islamic State, mwanamke huyo alikuwa peke yake wakati ndege za Jordan ziliposhambulia nyumba moja nje ya mji wa Raqqa.
Lakini maafisa mjini Washington na Amman wanasema kuwa hakuna thibitisho la mauaji yake kando na picha za nyumba iliokuwa imeharibiwa na kuyataja madai ya Islamic State kama propaganda za kutaka kuugawanya muungano huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni