27 Februari 2015
UZINDUZI WA KIVUKO
Leo Dkt.Magufuli amewaongoza wananchi wa Dsm kwenye majaribio ya uzinduzi wa Kivuko kipya Cha MV DAR ES SALAAM kitakachofanya safari zake kati ya Dsm na Bagamoyo, ambapo mamia ya wananchi wakiongozwa na Waziri Magufuli wamesafiri bure kutoka Dsm kwenda Bagamoyo na kurudi.
Kivuko hicho kimejengwa na kampuni ya Denmark na kwamba kimegharimu Sh7.9 bilioni.
“Kivuko hiki kitakuwa mkombozi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na kitakuwa kikifanya safari zake kuanzia Dar es Salaam hadi Bagamoyo,” amesema Dk Magufuli.
Dk Magufuli anesafiri watu wengine wapatao 300 kwenda Bagamoyo na kurudi Dar ES Salaam, wengine alioongozana nao ni katika kivuko hicho ni; Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi - Mhandisi Mussa Iyombe, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dsm, Balozi H.Mlango - M/Kiti Bodi ya TEMESA, Mkuu wa Mkoa wa Pwani - Mhandisi Everest Ndikilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TEMESA, Mkurugenzi Mtendaji TANROADS .
Awali Waziri Dk Magufuli aliahidi kufanya jitihada za kupunguza foleni jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kununua kivuko ambacho kitakuwa kinafanya safari kupitia Bahari ya Hindi Kutokea maeneo ya Feri(Dsm) mpaka Bagamoyo.
Dk Magufuli amesema sifa za kivuko hicho ni;
A) Kimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na kina mwendo (speed) kubwa kuliko vivuko vyote Tanzania.
B) MV Dar es Salaam, kina ghorofa mbili.
C) Kimetengenezwa kwa teknolojia hal ya juu (teknolojia ya kisasa)
D) Muonekano wa ndani ni wa kisasa yakiwamo makochi mazuri na life jacket.
E) Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria kati ya 306 hadi 400.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni