Image copyrightStatehouse TanzaniaImage captionDkt Magufuli amesema bado anatafuta watu wa kujaza nafasi nne
Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza baraza lake la mawaziri ambalo kwa sasa lina mawaziri 19, ingawa wizara ni 18. Mawaziri sita kati ya hao ni wanawake.
Waziri wa ulinzi nchini marekani Ash Carter anasema kuwa kikosi maalum cha jeshi la marekani nchini Iraq kitatumwa kuendesha oparesheni kadha dhidi ya Islamic State nchini Syria.
Bwana Carter aliiambia kamati ya bunge la Congress mjini Washington kuwa kikosi hicho kitafanya mashambulazi, kitawakomboa mateka na kuwakamata viongozi wa Islamic State.
Shirika la Umoja wa Mataifa linasema watu 40,000 wamekimbia makaazi yao kutokana na mapigano kati ya maafisa wa usalama kutoka maeneo mawili.
Msemaji wa umoja wa mataifa amesema watu 30 wameuawa katika makabiliano hayo yanayoendelea katika maeneo ya Galkayo, eneo lililoko katikati ya Somalia na Puntland Kaskazini .
Kumekuwepo mapigano ya muda mrefu ya kiukoo katika maeneo hayo mawili.
Umoja wa mataifa unasema wakimbizi hao wanahitaji vyakula misaada ya matibabu, maji na huduma za usafi.
Takriban watu 10 wamepigwa risasi na
kuawa baada ya makundi mawili kutofautiana kuhusu jogoo yupi aliyeibuka
mshindi katika vita katika jimbo la Guerrero Mexico.
Kundi la wapiganaji la Islamic State
limetoa taarifa kusema kuwa lilifanya mashambulio ya mjini Paris Ijumaa
usiku ambapo watu kama 127 waliuwawa.
Rais Hollande ameelezea
mashambulio hayo kuwa kitendo cha vita vilivotangazwa na IS ambao
alisema walipata msaada kutoka ndani ya nchi. Image copyrightPAImage caption
Shambulizi Paris
Ametangaza hali ya dharura.
Wanaume wanane
waliovaa vizibau vyenye mabomu walikufa kwenye mashambulio hayo katika
sehemu sita mbalimbali za mji mkuu wa Ufaransa.
Papa Francis kurahisisha sheria ya talaka miongoni mwa wakatoliki
Papa Francis
anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki
waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa
katika kanisa hilo .
Utafiti wa hivi
karibuni uliowachunguza wanafunzi 1000 Korea Kusini umebaini kuwa
asilimia 72 ya watoto wanapata simu wakifikia umri wa miaka 11 au 12.
Wapiganaji wa
kiislamu wa Alshabab wamesema katika maneno yao kuwa linawashikilia
mateka wa kivita kutoka Uganda waliowateka wakati wa mashambulizi ya
wiki iliyopita.