01 Desemba 2015

Je umetuma picha za utupu kwa simu? Tahadhari

Image copyrightAP
Image captionJe umetuma picha za utupu kwa simu? Tahadhari
Je umewahi kutuma picha za utupu kwa mpenzi wako ?
Je ulimshawishi akutumie ?

Ikiwa jibu lako ni ndio basi tahadhari.
Kwa mara ya kwanza mahakama imeamuru kulipwa kwa fidia na msichana mmoja ambaye alishurutishwa kutuma picha za utupu kupitia mtandao wa kijamii.
Hii ni kufuatia kesi ambapo msichana mmoja alishawishiwa kutuma picha zake za uchi kwenda kwa mwalimu wake.
Sasa inamaanisha kuwa yeyote ambaye atadhulumiwa kwa kushurutishwa kutuma au kupokea ujumbe unaohusu ngono au picha na kuathiriwa kisaikolojia kutokana na hilo anaweza kudai fidia.
BBC ilipata fursa ya kuzungumza na muathiriwa katika kesi ambapo muathiriwa mwenyewe hawezi kutajwa jina.
Image copyrightTHINKSTOCK
Image captionMahakama imeamuru kulipwa kwa fidia na msichana mmoja ambaye alishurutishwa kutuma picha za utupu kupitia mtandao wa kijamii.
Muathiriwa anasema kuwa akiwa bado kijana alifanya urafiki na mwalimu katika shule mpya.
Mwalimu hiyo William Whillock alikuwa naibu mkuu katika kitengo cha kulinda watoto katika shule hiyo na alikuwa na umri wa miaka 50 hivi wakati huo.
"Alikwa kama babangu," msichana huyo alisema.
"Alikuwa akiniambia kuwa kama nina shida yoyote niwe nikimpigia simu.''
Muathiriwa anasema kuwa akiwa shule, alikuwa akienda kwa ofisi yake kumueleza shida alizo nazo nyumbani.
Wakati uhusiano kati yao ulipokua zaidi mambo yakaanza kwenda mrama.
Image copyrightTHINKSTOCK
Image captionAnasema kuwa bwana Whillock angeweza kupigia simu au kumtumia ujumbe usiku wa manane akitaka amtumia picha zake za utupu.
Anasema kuwa bwana Whillock angeweza kupigia simu au kumtumia ujumbe usiku wa manane akitaka amtumia picha zake za utupu.
Akiwa na umri wa miaka kumi na nane muathiriwa alimtumia mwalimu picha zaidi akiwa nusu uchi.
Licha ya kumuambia atoe picha hizo kwa simu yake, simu yake iligunduliwa na mwalimu mwingine shuleni.
Bwana Whillock alikamatwa mbele ya wanafunzi na kukiri kumiliki picha za mwanafunzi alipofikishwa mahakamani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728