16 Desemba 2015

Kanisa kuandaa ibada ya Star Wars

Star WarsImage copyrightl
Image captionFIlamu ya The Force Awakens imezua msisimko mkubwa kote duniani
Kanisa moja mjini Berlin limetangaza kwamba litaandaa ibada maalum kabla ya Krismasi itakayoongozwa na filamu ya Star Wars.

Kuna msisimko mkubwa Ujerumani kabla ya kuzinduliwa nchini humo kwa filamu mpya ya mwendelezo wa filamu za Stars Wars kwa jina The Force Awakens Alhamisi.
Kanisa la Zion Church, lililoko eneo la katikati mwa jiji la Mitte, limetumia msisimko huo kuandaa ibada ya kipekee ya Jumapili asubuhi.
Ibada hiyo itaongozwa na filamu nambari nne ya Star Wars kwa jina Return of the Jedi.
Filamu hiyo ilizinduliwa mwaka 1983, na wale watakaohudhuria ibada hiyo wataonyesha sehemu za filamu hiyo.
Wazo la kuandaa ibada hiyo lilitokana na wahubiri wawili ambao wanajifunza kuhubiri, Ulrike Garve na Lucas Ludewig, kanisa hilo limesema kwenye tovuti yake.
Wanalinganisha filamu hiyo ya George Lucas na matukio kwenye Biblia.
“Katika tukio moja Luke Skywalker ianavutwa upande wa mfalme, wa maovu,” anasema Ludewig, ambaye ameelezwa na kanisa hilo kuwa mwanatheolojia na mtaalamu wa Star Wars.
"Luke anapinga kwa kusema: Sitawahi kujiunga na upande wa giza.”
Hilo anasema linalingana na sehemu kwenye kitabu cha Warumi: “Msiruhusu maovu yawatawale, lakini shindeni uovu kwa kutenda mema.”
Star WarsImage copyrightGetty
Image captionFilamu mpya ya Star Wars ilionyeshwa mara ya kwanza mjini Los Angeles Jumatatu
Bi Garve anasema wale watakaotokea wakiwa wamevalia mavazi sawa na yanayovaliwa kwenye filamu hizo ana nafasi ya kuingizwa kwenye shindano la kushindania tiketi za kutazama filamu ya sasa ya The Force Awakens.
Nchini Kenya, filamu hiyo mpya ya Star Wars inatarajiwa kuanza kuonyeshwa Kenya Desemba 18.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728