27 Agosti 2015

HAPAPATOSHI NDANI YA JIJI LA DAR

Msanii wa kizazi kipya

Saa 2 zilizopita
Neno moja huweza kubadilisha maisha ya mtu, hayo yamemkuta msanii wa muziki nchini Tanzania
Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Abubakar Shaaban Katwila almaarufu Q Chillah aliyekuwa ameathiriwa na dawa za kulevya kiasi cha kushindwa kuendelea kuiburudisha hadhira, ameamua kuitoa siri yake kwa BBC namna alivyoweza kuachana na uraibu, sababu kubwa ni neno aliloguswa kutoka kwa bintiye.
Sikiliza mahojiano yake na Anord Kayanda

Uchaguzi 2015: Jackline Wolper Atangaza Kujiita ‘Jackline Lowassa

Uchaguzi 2015: Jackline Wolper Atangaza Kujiita ‘Jackline Lowassa’
Mastaa wa Bongo Movies, Jackline Wolper , Aunt Ezekiel na Shamsa Ford ambao wamekuwa wakimuunga

Rose Ndauka: Nipo Tayari Kuolewa na Yeyote!

Rose Ndauka: Nipo Tayari Kuolewa na Yeyote!ROSE Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ amesema kama mwanamke aliyekamilika na mwenye kuhitaji heshima katika jamii, yupo tayari kuolewa na kuishi kama mama na mwanaume yeyote.

Muuaji ajiua Marekani

Polisi nchini Marekani imesema muuaji wa Waandishi wawili wa habari nchini Marekani amefariki.
Ujumbe unaoonekana kutumwa na mtu aliyekuwa na silaha nchini Marekani na kuwaua kwa risasi watangazaji hao wawili wa televisheni wakati wa matangazo ya moja kwa moja unaashiria kwamba alikuwa na uchungu kwa kinachoonekana kuwa ubaguzi wa rangi.

Je hali ya wachimba dhahabu TZ itaimarika ?

Je hali ya wachimba dhahabu TZ itaimarika ?

Marekani yamuonya rais Salva Kirr

 
Salva Kiir
Marekani imemuonya rais wa Sudan Kusini Salva Kirr, kuheshimu na kutekeleza mkataba wa amani aliousaini siku ya Jumatano mjini Juba.

Polisi wanasa sehena ya Silaha Kenya

 
Silaha zilizonaswa Garisa
Maafisa wa Ulinzi wa Kenya wamenasa shehena kubwa ya silaha, kufuatia operesheni ya kuwasaka wapiganaji wa Al Shabaab Kaskazini mwa Kenya.

Usain Bolt bingwa wa dunia wa mita 200

 
Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt, ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu, katika mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea mjini Beijing nchini Uchina.

Pistorius kusalia gerezani zaidi

Kamati itakayoamua ikiwa mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, anapaswa kuachiliwa kutoka gerezani, inatarajiwa kukutana tarehe 18 mwezi ujao.

Miili ya wahamiaji yapatikana Austria

 
Lori lililokuwa na miili ya wahamiaji
Maafisa wa serikali ya Austria wamesema kuwa wa wamegundua miilli ya wahamiaji kadhaa ambayo iliachwa ndani ya lori moja katika mkoa wa Burgenland, karibu na mpaka wa Hungary.

Wanawake waoana nchini Tanzania,kunani?

Wegesa na Nyanswi. Ni wanawake wawili kutoka kwa jamii ya Wakuria.
Wameoana kwa miaka 15.

Waandishi 2 wauawa wakiwa hewani Marekani

Waandishi wawili wa habari wamepigwa risasi katika jimbo la Marekani la Virginia wakati wakifanya mahojiano ya moja kwa moja ya runinga.

Ray Aangua Kilio Ukumbini!

Ray Aangua Kilio Ukumbini!BONGE la soo! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza kufananishwa na marehemu Steven Kanumba.

24 Agosti 2015

Umoja wa Ulaya na tatizo la wahamiaji

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamezitaka nchi za Umoja wa Ulaya kufanya kazi pamoja kuweza kukabiliana na tatizo la wahamiaji.
Katika taarifa yao ya pamoja kwa vyombo vya habari mjini Berlin, Kansela Angela Merkel amesema kanuni zilizokuwepo sasa kama vile kuwasajili wahamiaji, hazifuatwi.
Kwa upande wake Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaka mgawanyo sawa wa wanaoomba hifadhi, kati ya mataifa wanachama.

Uingereza na uhamiaji haramu

Serikali ya Uingereza itatangaza leo Jumanne mapendekezo mapya ya kukabiliana na suala tata la uhamiaji.
Wahamiaji ambao watapatikana wakifanya kazi kinyume na sheria nchini Uingereza na Wales, watakabiliawa na hukumu ya hadi miezi sita gerezani na kupigwa faini ya fedha nyingi.

Tanzania na ugonjwa wa Sickle Cell.

Video ya hali ya juu mp3 (3.4 Mb)

Tanzania na ugonjwa wa Sickle Cell.

Saa 7 zilizopita
Tanzania ni nchi ya tano Duniani kwa kuwa na watu wenye ugonjwa wa Sickle Cell.
Utafiti unaonyesha kuwa kila mwaka nchini Tanzania takribani watoto elfu kumi na moja huzaliwa na ugonjwa huo.
Moja ya sababu ya ongezeko hilo ni uelewa mdogo juu ya ugonjwa huo unaohusiana na seli za damu kuwa katika umbo nusu.
Sikiliza ripoti ya Arnold Kayanda kuhusiana na ugonjwa huo.

Arsenal , Liverpool hakuna mbabe

 
Christian Benteke mwenye jezi nyeusi akijaribu kufunga goli bila mafanikio 
 
Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech aliokoa mara mbili mipira ya hatari iliyokuwa ikielekea langoni mwake na kuisaidia timu yake kupata alama moja katika mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool.

Kampeni za Uchaguzi mkuu zaanza Tanzania

Video ya hali ya juu mp3 (1.9 Mb)

Kampeni za Uchaguzi mkuu zaanza Tanzania

24 Agosti 2015 Imebadilishwa mwisho saa 01:37 GMT
Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania zimeanza rasmi juzi. Oktoba 25 wananchi watapiga kura kuchagua madiwani, wabunge na Rais
Sikiliza taarifa ya Sammy Awami aliyehudhuria uzinduzi wa kampeni za Chama tawala CCM.

Wachina wanaozungumza kiswahili China

Video ya hali ya juu mp3 (2.1 Mb)

Wachina wanaozungumza kiswahili China

24 Agosti 2015 Imebadilishwa mwisho saa 16:33 GMT
Fatuma Halnur ni baadhi ya Wachina hapa wanaozungumza kiswahili pia. Fatuma, ambaye ni muislamu, ni mwanafunzi katika chuo cha Lugha za kigeni cha Beijing...John Nene amekutana na Fatuma mjini Beijing, na kwanza akamuuliza mbona ameamua kujifunza kiswahili.

Mourinho aanza tambo:

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema matokeo ya timu yake dhidi ya West Brom yatawanyima raha wabaya wao.
Ameyasema hayo baada ya kupata ushindi wa kwanza tokea msimu mpya wa ligi ya England ianze.
Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, Chelsea iliibuka kidedea kwa jumla ya bao 3-2 dhidi ya West Brom na kushuhudia nahodha wake John Terry akilimwa kadi nyekundu katika dakika ya 54 ya mchezo baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon. Ushindi huu ni wa kwanza kwa Chelsea baada ya kufanya vibaya kwenye michezo miwili ya awali. Lakini pia hii ni mara ya kwanza kwa matajiri hao wa jiji la London, kufanya vibaya katika michezo miwili mfululizo ya awali katika kipindi cha miaka 17.

22 Agosti 2015

Rais Nkurunziza aomba utulivu Burundi

Nshimirimana
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameomba utulivu baada ya wapiganaji waliovalia magwanda ya kijeshi kumuua mmoja ya majenerali walio na ushawishi mkubwa serikalini.

Chad:Boko Haram lina kiongozi mpya

 
Rais wa Chad Idriss Deby 
 
Kundi la wapiganaji wa Boko haram kutoka Nigeria huenda limepunguzwa makali kulingana na rais wa Chad Idriss Deby.

Museveni amsuta Raila kuhusu Sukari

Museveni amusuta Raila kuhusu Sukari
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemsuta kiongozi wa upinzani wa Kenya, Raila Odinga, kwa kupinga mkataba wa uuzaji wa sukari uliotiwa sahihi majuzi.
Museveni alisema kuwa Odinga hafaaamu anachokisema.
''hata ndugu yangu odinga anazungumzia maswala ya sukari,bila kufahamu ukweli wa maswala hayo'' Museveni.

15 Agosti 2015

Miaka 130 jela kumuambukiza mtoto Ukimwi

miaka 130 jela kumuambukiza mtoto Ukimwi
Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 130 jela kwa kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 ukimwi.

Je unandoto ya kuwa mjasiria mali?

Watu wengi siku hizi na haswa vijana huwa wakishahitimu chuoni wanatafuta ajira kwa kipindi kirefu na hatimaye wanakata tamaa.

Kiongozi wa IS alidaiwa kum'baka mateka

Kayla Mueller
Mfanyikazi wa huduma za misaada kutoka Marekani ambaye aliuawa mnamo mwezi februari akiwa mateka wa kundi la Islamic State nchini Syria alinyanyaswa kijinsia na kiongozi wa kundi hilo Kulingana na maafisa wa Marekani.

RIPOTI ZA MOJA KWA MOJA ZA MECHI ZA LIGI KUU YA UINGEREZA

RIPOTI ZA MOJA KWA MOJA ZA MECHI ZA LIGI KUU YA UINGEREZA


EPL
18.55pm:Matokeo ya mechi za EPL
Southampton 0 - 3 Everton
Sunderland 1 - 3 Norwich
Swansea 2 - 0 Newcastle
Tottenham 2 - 2 Stoke
Watford 0 - 0 West Brom
West Ham 1 - 2 Leicester

18.51pm:Na Mechi inakamilika ikiwa Tottenham 2 Stoke 2.

Idadi ya waliokufa China yaongezeka

kufa China yaongezeka 
 
Idadi ya watu waliouawa kwenye milipuko mikubwa katika bandari ya Tinjian nchini China siku ya Jumatano imeongezeka hadi watu 85.

Barcelona yacharazwa 4-0 na Bilbao

Kilabu ya Athletico Bilbao iliwawacha mabingwa wa kombe la vilabu bingwa Ulaya mdomo wazi katika awamu ya kwanza ya mechi ya kombe la Super Cup huku Aritz Aduriz akicheka na wavu mara tatu katika mechi isio ya kawaida.

Al Qaeda:Mwana wa Bin Laden atoa ujumbe

Osama Bin Laden 
 
Kundi la kigaidi la A Qaeda limetoa ujumbe wa sauti ambao unadai kwamba umetoka kwa Hamza Bin Laden ,mwana wa Osama Bin Laden.

Umri ni miaka 26 lakini umbile ni miaka 10

hakuna ndevu na sauti yake ni nyororo utadhania ni mtoto! 
 
Ni mwanaume kwa kila hali ya siha ila sifa za maumbile yake ni sawa na yale ya mtoto wa miaka 10.
Si jambo la kujivunia kuwa wewe huzeeki ?

Mourinho:Daktari'mjinga' hatakuwepo uwanjani

Dakta Eva Carneiro amehudumu Stamford bridge kwa miaka 5 sasa
Meneja wa Chelsea manager Jose Mourinho amekariri msimamo wake dhidi ya kitengo cha utabibu cha timu yake.

Japan inajutia vita vya pili vya dunia

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ameeleza kusikitishwa kwake na mateso
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ameeleza kusikitishwa kwake na mateso na kujitolea kwa watu wengi wakati wa vita vya pili vya dunia.

13 Agosti 2015

Mourinho amtimua daktari wa timu

Eva Carneiro daktari wa Chelsea aliyeketi kushoto
Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho anapaswa kuomba msamaha kwa daktari wa timu Eva Carneiro ''kwa kumfedhehesha hadharani'' daktari wa zamani wa

Fidel Castro aandika barua ya wazi Cuba

Rais wa zamani wa Cuba,Fidel Castro
Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro ametimiza umri wa miaka 89 kwa kuandika barua ya

Ugiriki yajitathmini na madeni kimataifa

Kumekuwa na majadiliano makubwa katika bunge la

Chachu ya kutuliza maumivu yapatikana

Wanasayansi nchini Marekani wamesema kuwa wamefanikiwa kutengeneza chachu yenye vina saba vinavyoweza kupunguza maumivu kwa

Jack Wilshere mapema zaidi

Jack Wilshere
Meneja wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amesema kuwa kiungo wa klabu yake Jack Wilshere anatarajiwa kurejea tena dimbani wiki mbili zijazo baada ya

Mtoto apata mtoto Paraguay.

Kampeni imeanzishwa kupinga ubakaji kwasababu ya kisa cha binti huyo.
Binti wa miaka kumi na mmoja nchini Paraguay aliyedai kubakwa na baba yake wa kambo amejifungua mtoto wa kike baada ya

David De Gea aufungukia uongozi

David De Gea
Mlinda mlango wa Manchester United David De Gea ameuambia uongozi wa klabu yake kuwa ''hakutaka kucheza'' kabla ya

05 Agosti 2015

Mayweather kupanda ulingoni septemba

Floyd Mayweather
Bondia Floyd Maywether atapanda tena ulingoni mwezi Septemba 12 mwaka huu kuzipiga na Andre Berto.

Wengi wavutiwa na muujiza Mali

Mali
Maelfu ya raia katika mji mkuu wa Mali Bamako wanaendelea kufurika ili kujionea kile kilichotajwa kuwa muujiza wa kidini katika ukuta mmoja ambao ulionekana wikiendi iliopita.

China ni haramu kuhifadhi mayai ukiwa hujaolewa

Serikali ya China imepiga marufuku uhifadhi wa mayai kwa wanawake ambao hawajaolewa.
Mjadala mkali umeibuka nchini China baada ya serikali kupiga marufuku kwa uhifadhi wa mayai kwa wanawake ambao hawajaolewa.

Ajali:Polisi taabani kwa kudanganya Kenya

Polisi wajipata pabaya kwa kudanganya kuhusu ajali iliyosababisha kifo Kenya
Shinikizo la kutaka Pasta mmoja maarufu nchini Kenya akamatwe limeanza kushika kasi baada ya uchunguzi wa mwanzo kuonesha kuwa alikuwa akiendesha gari aina la

Wakimbizi wa Somalia warejeshwa kwao

Wakimbizi wa Somalia warejesha kwao
Wakimbizi wa kwanza 100 wamerejeshwa Somalia kufuatia makubaliano kati ya Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia maswala ya

Je unataka kuishi maisha marefu duniani ?

Ukila vyakula vilivyotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu; 'Utafiti'
Je unataka kuishi maisha marefu duniani ?
Utafiti mmoja uliofanywa nchini China umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu.

UN:Shambulio la Burundi lichunguzwe

Mbonimpa
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametaka uchunguzi wa kina ufanywe kwa shambulio lililofanywa dhidi ya mwanaharakati wa haki za

Wasifu wa Edward Lowassa

Je unamfahamu Edward Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania ?
Umoja usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA), baada ya kusubiri kwa muda hatimaye umemtangaza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728