27 Agosti 2015

Marekani yamuonya rais Salva Kirr

 
Salva Kiir
Marekani imemuonya rais wa Sudan Kusini Salva Kirr, kuheshimu na kutekeleza mkataba wa amani aliousaini siku ya Jumatano mjini Juba.

Rais Kirr, alikuwa amekataa kusaini mkataba huo wiki iliyopita mjini Adis Ababa Ethiopia.
Lakini, licha ya kusaini mkataba huo, ameelezea wasi wasi wake kuhusiana na masuala kadhaa ya mkataba huo, hasa kugawana madaraka na waasi.
Mkataba huo unanuiwa kumaliza mzozo uliodumu kwa muda wa miezi Ishirini.
Usitishwaji wa mapigano unapaswa kutekelezwa katika muda wa saa 24 na majeshi ya kigeni yanapaswa kuondoka nchini humo.
Image copyright Reuters
Image caption Sudan Kusini
Hakuna wanajeshi watakaoruhusiwa kufika karibu na mji mkuu Juba.
Kiir ambaye alikabiliwa na shinikizo za kimataifa kuidhinisha mkataba huo anatarajiwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kiongozi wa waasi Riek Machar

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728