Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt,
ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu, katika mashindano ya riadha ya
dunia yanayoendelea mjini Beijing nchini Uchina.
Bolt alitimuka mbio hizo kwa muda wa sekunde 19.55 na kunyakulia taifa lake medali nyingine mbali na kuandikisha rekodi ya kuwa mwanariadha kasi zaidi duniani katika mbio za masafa mafupi.
Ushindi huo ni wa kumi kwa mwanariadha huyo kutoka Jamaica na ni ya nne mfululizo katika mbio hizo za dunia.
Justin Gatlin wa Marekani, pia alishinda medali ya fedha katika mbio za mita mia moja, alimaliza wa pili akifuatwa na
Gatlin alitumia sekunde 19.74.
Shericka Jackson wa Jamaica naye alizoa medali ya shaba kwa kutumia muda wa sekunde 49.99.
Bingwa wa dunia wa mbio mita mia nane kwa kina dada, Mkenya Eunice Sum, nusura ayaage mashindano hayo pale alipomaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio za mchujo.
Hata hivyo Sum, alinusurika pale muda wake wa dakika 1.57.56 ulikuwa wa kasi zaidi kati ya wale waliomaliza katika nafasi ya tatu katika makundi yao, na hivyo kufuzu kwa fainali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni