Hemoroid ni ugonjwa unaoujulikana pia kama ugonjwa wa vifundo katika njia ya haja kubwa. Hata hivyo, huwa na majina mengi kama bawasili ukisababishwa na kulegea kwa misuli laini ya mishipa hiyo ya damu, hivyo mishipa husika hutanuka kuliko kawaida na kulegea, kisha kutokeza katika njia ya haja kubwa ikiambatana na ukuta wa njia hiyo. Sababu hasa ya kulegea kwa mishipa hiyo hazijaweza kueleweka.
Lakini, mabadiliko yafuatayo huchangia kwa kiasi kikubwa mtu kupatwa na hemoroid nayo ni; kupata choo kigumu mara kwa mara, kuharisha mara kwa mara, kukaa kwa muda mrefu, kuwa na uzito mkubwa kuliko inavyotakiwa (BMI>30), kukohoa mara kwa mara, uvimbe tumboni, kuzaa watoto wenye uzito mkubwa mfano zaidi ya kilo nne.
Baadhi ya dalili za ugonjwa huu ni kuhisi kushuka kwa fundo la sehemu ya haja kubwa wakati wa kupata choo, ambalo linaweza kurudi lenyewe ndani baada ya kupata choo, au inabidi kulirudisha kwa kidole, au kushindikana kabisa kurudishwa kwa kidole na kubaki likininng’inia nje kwa muda mrefu.
Nyingine ni kutokwa damu wakati wa haja kubwa inayoweza kuchafua nguo za ndani, wakati mwingine damu hutoka kwa wingi na mfululizo bila kuganda, hvyo uhatarisha maisha.
Uchunguzi na matibabu
Vipimo kama proctoscopy (kuchuguza kwa chombo maalumu chenye mwanga), proctosigmoidoscopy huweza kufanyika, pia kuwekewa dawa maalumu, kisha kupiga ex-ray (barium enema). Kwa watu walio na umri mkubwa, mfano zaidi ya miaka 50 ni muhimu zaidi kuchunguzwa kitaalamu kwani hilo ni kundi lililo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya njia ya haja kubwa. Mtu anaweza kufikiri ni tatizo dogo, kumbe anasumbuliwa na saratani ya njia ya haja kubwa, hivyo matibabu hubadilika.
Matibabu
Iwapo hemoroids hazijawa kubwa, yaani zipo katika hatua ya kwanza au ya pili ni muhimu kutibu vinavyochochea ugonjwa kama vilivyoainishwa hapo juu. Iwapo tatizo lipo katika hatua ya tatu au ya nne, au matibabu tajwa hapo juu yameshindikana, upasuaji ndiyo matibabu sahihi ya ugonjwa huu.
05 Oktoba 2014
Ugonjwa wa hemoroid (haenorrhoids)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni