11 Oktoba 2014

HAWAFAI KABISA: Lampard akoshwa na Costa, Fabregas

FRANK Lampard hayupo ndani ya kikosi cha Chelsea kwa mara ya kwanza baada ya miaka 13. Siku hizi anavaa jezi ya Manchester City. Lakini bado anatupa jicho la umbea katika timu yake ya zamani na anakwambia Cesc Fabregas na Diego Costa hawafai hata kidogo!
Chelsea imetumia zaidi ya Pauni 100 milioni kuwachukua Filipe Luis, Cesc Fabregas, Diego Costa, Didier Drogba na Loic Remy na imewaruhusu Ashley Cole, David Luiz, Samuel Eto’o na yeye kuondoka Stamford.
Lakini Lampard ameonyesha kukoshwa vilivyo na viwango vinavyoonyeshwa na Costa na Fabregas ambao pia ni nyota wa kimataifa wa Hispania.
Nyota hao wameonyesha maelewano makubwa uwanjani na kuweika Chelsea kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointi 19 huku wakiwa hawajapoteza mechi.
“Nimetazama mechi zao tokea mbali na pia nimecheza dhidi yao. Hakuna yeyote kati yao ambaye amenishangaza. Cesc Fabregas nimecheza dhidi yake akiwa Arsenal. Anaijua Ligi Kuu ya England na ni mchezaji wa kiwango cha dunia,” alisema Lampard.
“Tulimtazama Diego Costa kabla hatujacheza na Atletico Madrid pambano la nusu fainali Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu uliopita. Tulitazama video zake na tungeweza kutazama hata kwa saa tatu jinsi alivyokuwa anakimbia, jinsi alivyokuwa anafunga mabao na kila kitu alichokuwa anakifanya uwanjani. Niliona kuwa alikuwa bonge la mchezaji na Chelsea hatimaye ilimsajili,” aliongeza Lampard.
Tayari Costa ameivamia kwa fujo Ligi Kuu ya England huku akiwa amefunga mabao tisa kufuatia uhamisho wake wa Pauni 32 milioni kutoka Atletico Madrid ambayo aliipatia ubingwa wa La Liga msimu uliopita huku pia akiifikisha fainali za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Wakati huo huo, Fabregas amepiga pasi saba za mabao huku pasi moja akiipika katika bao la pili la ushindi la Costa dhidi ya timu yake ya zamani, Arsenal Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Stamford Bridge.
Wengi wanatabiri kuwa, Fabregas atachukua umuhimu wa Lampard katika kikosi cha Kocha Jose Mourinho ingawa Lampard anakumbukwa kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Chelsea akiwa na mabao 211 katika kikosi hicho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728