Njombe. Vijana wametakiwa kuisoma Katiba Inayopendekezwa kwa umakini na kuvielewa vipengele vilivyopo katika Ibara zote ili wafanye uamuzi sahihi.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana Mkoa wa Njombe, Luca Mgaya alitoa rai hiyo mjini hapa jana.
Alisema vijana wakiielewa Katiba wataepuka vishawishi vya nini wafanye kutoka katika makundi mbalimbali, yakiwamo ya kisiasa.
Alisema vijana wana wajibu wa kuhakikisha wanafuatilia vyema Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa kwa kupata nakala yake na kuisoma ili kuelewa mambo yaliyomo.
Alisema vijana wana wajibu wa kuhakikisha wanafuatilia vyema Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa kwa kupata nakala yake na kuisoma ili kuelewa mambo yaliyomo.
Alisema vijana wanapaswa kujiepusha kushikiwa akili na makundi yanayopita kuwashawishi kuikubali rasimu hiyo au kuikataa, badala yake waisome na kutoa uamuzi wao.
“Kuna makundi yanasema kuna vipengele vya msingi vimeondolewa katika Rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba, wengine wanasema Rasimu ni nzuri, iungeni mkono.
“Sisi vijana kabla ya kufanya uamuzi wowote, lazima tuipate nakala ya Rasimu hiyo tuisome kipengele kwa kipengele ili tuelewe kilichomo ndipo tufanye uamuzi,” alisema.
Alisema kama watabaini kuna vipengele vya msingi vimeondolewa katika Rasimu hiyo, watahoji vimeondolewa kwa sababu gani ili kupata ufafanuzi.
Pia aliwataka vijana kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Desemba mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.
Aliwataka vijana kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pindi litakapoanza kuboreshwa ili waweze kutumia vyema haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni