Kweli dunia ina mambo! Kuna watu wanajaribu kutumia kila fursa
inayopatikana kujinufaisha kwa kupata fedha hata ziwe ‘chafu’, kwao kitu
cha maana ni kupata utajiri kwanza.
Kundi la watu wanaofanya biashara ya kusafirisha
watu, wamekuwa wakitumia fursa ya ukosefu wa ajira kama chambo cha
kuwanasa vijana na kuwaingiza kwenye biashara haramu kama ukahaba.
Hivi karibu kundi hilo linalosafirisha watu
lilipita katika vyuo vikuu kadhaa nchini Uganda na kuwaahidi wanafunzi
kuwa lingewatafutia kazi Ulaya na Marekani, kwani lina uzoefu wa kutosha
na kazi hiyo.
Mmoja wa vijana ‘waliobahatika’ kupata nafasi ya kwenda Ulaya kufanya kazi ni Sunday Bekunda (25), mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala.
Mmoja wa vijana ‘waliobahatika’ kupata nafasi ya kwenda Ulaya kufanya kazi ni Sunday Bekunda (25), mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala.
Kwa bahati mbaya ‘neema’ ya kwenda Ulaya iligeuka
balaa baada ya kutekwa na kulazimishwa kufanya ngono na wanawake
mbalimbali huku akirekodiwa kwenye kamera za video.
“Ilikuwa ni Januari 2013, nilipokutana na mwanaume
mmoja anayeitwa Charles kutoka katikati ya Jiji la Kampala, ambaye
aliniahidi kunipeleka Kenya kufanya kazi katika kiwanda.
“Sikujua kuwa Charles alikuwa msafirisha watu. Alikuwa anaonekana kama mzazi wa makamo aliyefanya kazi kwa miaka mingi.
“Nilifungua moyo wangu na kumweleza changamoto
nyingi ninazopitia na namna nilivyo hangaika kutafuta kazi ili nipate
fedha za kulipia masomo ya ziada. Kwa kifupi ni kama nilikuwa namwambia
Charles kuwa sikuwa natafuta kazi bali nilikuwa nataka kazi yoyote.”
Safari ya Kenya
“Siku iliyofuata nilikuwa tayari kwa safari na
nilimkuta Charles akiwa kwenye gari la binafsi aina ya Toyota Noah.
Alikuwa pamoja na wasichana sita na wavulana wawili. Alituambia kuwa
tutaingia Kenya kwa kupitia mpaka usio rasmi unaoitwa Chepskunya.
“Tukiwa njiani, Charles alikuwa anaongea sana na
kutusisitizia kuwa ‘tusimwangushe’ tukifika huko. “Tulipofika Kenya
walituchukua na kutuingiza kwenye nyumba moja nzuri ya makazi ya watu,
hapo tulikutana na wenzetu 15, wavulana wawili kutoka Rwanda na Wakenya
13.”
Kutekwa
“Charles alituacha hapo tukiwa chini ya mwanamke
mmoja na wanaume wanne wenye miili iliyojengeka vyema. Watu hao walianza
kutupiga makofi na kutulazimisha tuvue nguo. Ndipo nilipobaini kuwa
kilichoonekana kama ni safari sasa imegeuka utekaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni