Je,katika utamaduni wenu kiongozi wa kijiji,mganga wa kienyeji na mkulima mashuhuri huzikwa vipi?.
katika kisa cha kushangaza ,wana kijiji wa Eshikombelo katika kaunti ya kakamega nchini kenya wanasema kuwa iwapo marehemu angekuwa mzee Adriano Aluchio angefanyiwa maziko ya kipekee.
Kulingana na gazeti la Standard nchini kenya,maelfu ya wanakijiji wa eneo hilo walihudhuria mazishi ya marehemu Aluchio ili kumpa heshima yake ya mwisho mzee huyo wa miaka 62.
lakini wengi wao walitaka kushuhudia sherehe ya kipekee ya Idakho.
Watu wa makabila madogo ya Bukusu,Idakho,Tachoni na Kabras katika kabila la Waluhya wanaamini kwamba kuwazika watu mashuhuri wakiwa wameketi ni ishara ya heshima kubwa sana.
''Tulipata tamaduni hizi na hivyobasi ni sharti tuishi nazo'' alisema Mzee Museve Mwidakho.
Mwidakho ambaye ni mzee wa ukoo wa kabila dogo la Idakho ambako marehemu Aluchio anatoka anasema kuwa utamaduni huo unalenga kuwashirikisha wafu na watu walio hai.
Anasema kuwa utamaduni huo ulianzishwa na Nabongo Mumia wa jamii ya Wanga na hadi leo umeigwa na makabila mengine madogo.
Anasema kuwa kumzika mtu akiwa ameketi pia kunafukuza mapepo wachafu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni