Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa Diego Costa ni mshambuliaji hatari na kwamba mshambuliaji huyo wa Chelsea ni tishio kubwa kwa kikosi chake katika mechi ya Leo itakayochezwa katika uga wa stamford Bridge.
Kilabu zote mbili hazijafungwa tangu msimu huu wa ligi uanze,lakini Chelsea iko juu ya Arsenal kwa pointi sita.
Costa aliyenunuliwa kwa kitita cha pauni millioni 32 kutoka kilabu ya Uhispania ya Atletico Madrid,amefunga mabao 8 katika mechi 6 za ligi ya Uingereza alizoshiriki.
''Costa ana kila kitu cha mshambuliaji,anajitolea na yuko tayari kufunga bao'',alisema Wenger.
Wenger anahisi matumaini kwamba huenda Arsenal ikaishangaza Chelsea ilio katika kilele cha jedwali la ligi ya Uingereza ikiwa na pointi 16 kati ya 18.
Msimu uliopita Arsenal ilipata kichapo cha mabao 6 kwa 0 katika mechi iliochezwa katika uga wa Stanford Bridge huku Wenger akiweka rekodi ya kuisimamia kilabu hiyo kwa mechi yake ya1000.
Kwa upande wake Mourinho anatarajia ushindani mkali kutoka kwa Arsenal na amejitayarisha vilivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni