Maafisa wa usalama nchini Yemen
wanasema waasi wa kundi la Houthi wameshikilia maeneo kadhaa ya mji wa
tatu kwa ukubwa wa Taiz, ukiwemo uwanja wa ndege.
Taiz ni mji ambao unapakana na mji mkuu wa Sanaa na mji wa kusini wa Aden.Umekuwa ni mji ambao una vikosi vitiifu kwa rais Abd Rabbuh Mansour Hadi.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajia kukutana kwa dharura hii leo kujadili kuzorota kwa usalama nchini Yemen, ambako waasi wa Houthi wanatawala eneo kubwa la nchi.
Kikao hicho cha baraza la usalama kimeombwa kuitwa na rais Hadi ambaye mwezi uliopita alikimbilia mjini Aden kutoka mji mkuu wa Sanaa.
Awali wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitangaza kuwaondosha maafisa wake mia moja waliosalia nchini Yemen kwa sababu za kiusalama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni