Waziri wa watumishi wa serikali wa Afrika Kusini, Collins Chabane, pamoja na walinzi wake wawili wamekufa kwenye ajali ya gari.
Gari lao liligongana na lori katika mji wa Polokwane, kaskazini-mashariki mwa nchi.
Bwana Chabane alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama tawala cha ANC na mshirika mkubwa wa Rais Jacob Zuma.
Aliongoza matayarisho ya mazishi ya Nelson Mandela.
Rais Zuma amesema ameshtushwa na kuskitishwa sana na kifo cha rafiki yake ambacho alisema kimeacha pengo kubwa serikalini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni