Mabingwa wa ligi ya Uingereza
Manchester City watamuuza Yaya Toure msimu huu katika mpango unaolenga
kuwauza wachezaji wengine wa kilabu hiyo kwa lengo la kununua wachezaji
chipukizi watakaoongozwa na mchezaji Kevin De Bruyn wa Wolfsburg.
Kushindwa
kwa kilabu hiyo na Barcelona katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali ya
kombe la vilabu bingwa Ulaya kumethibitisha kwamba mabadiliko makubwa
yanahitajika katika kilabu hiyo.Katika wachezaji kumi na moja walioanzishwa katika mechi dhidi ya Barcelona ni Sergio Aguerro mwenye umri wa maka 26 aliye chini ya umri wa miaka 27.
Huku Aguerro,Joe Hart,Vincet Kompany,Fernandinho na David Silva wakiwa na maisha marefu katika kilabu hiyo ,waliosalia huenda wakauzwa.
Hii inamaanisha kwamba Yaya Toure,Bacary Sagna,Martin Demichelis,Alkesandar Kolarov ,Samir Nasri na James Milner ambaye kandarasi yake inaisha hatma yao haijulikani.
Kati ya wachezaji ambao hawakuanzishwa katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumatano usiku,Gale Clichy,Pablo Zabaleta,Jesus Navas,Fernandinho,Steven Jovetic na Edin Dzeko huenda pia wakauzwa.
Frank lampard amesema kuwa anaondoka ili kujiunga na kilabu ya New York City nchini Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni